Connect with us

EPL

DE GEA: BRUNO HAUSTAHILI KUWA NAHODHA.

Nahodha wa zamani wa Manchester United amemtania rafiki yake wa karibu Bruno Fernandes kwa kuandika kuwa hakustahili kuwa nahodha wa kikosi hicho.

Nahodha wa zamani wa Manchester United na golikipa wa zamani wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Hispania, David De Gea kupitia ukurasa wa Instagram amemwambia Bruno Fernandes kuwa yeye sio nahodha sahihi wa klabu hiyo na hakustahili kuwa nahodha.

Wewe sio nahodha sahihi.

Nahodha wa zamani wa Manchester United, David De Gea.

De Gea ameyasema hayo kwenye picha aliyoichapisha Bruno kwenye ukurasa wa Instagram mara baada ya Manchester United jana kupata ushindi wakiwa ugenini wa goli 0-1 dhidi ya Fulham. Goli ambalo lilifungwa na kiungo mshambuliaji raia wa Ureno ambaye pia ni nahodha wa klabu hiyo Bruno Fernandes.

Bruno alikabidhiwa kitambaa cha unahodha baada ya kuvuliwa kitambaa hicho Harry Maguire mapema mwanzoni mwa msimu huu.

Bruno Fernandes na David de Gea ni marafiki sana na ameandika maneno hayo ili kutaka kuwaonyesha wale wasio na imani na Bruno kuwa nahodha wa kikosi hicho kuwa anastahili baada ya kuipatia ushindi klabu yake hapo jana. Hii imetokana na baadhi ya wachambuzi akiwemo mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Roy Keane kusema Bruno hastahili kuwa nahodha wa Manchester United.

Bruno hana sifa ya kuwa nahodha, ana lia lia na kulalamika kila muda.

Roy Keane alisema baada ya Mchezo wa Manchester United dhidi ya Manchester City kutamatika.

Makala Nyingine

More in EPL