Connect with us

CAF Women Champions League

JKT QUEENS KUIVAA MAMELODI LEO WCAFCL.

Nahodha wa klabu ya JKT Queens Amina Bilali amesema wamejiandaa vyema kuikabili Mamelodi Sundowns hii leo.

23:00 JKT QUEENS vs MAMELODI SUNDOWNS

IVORY COAST

Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa upande wa wanawake inatarajiwa kuanza hii leo nchini Ivory Coast. Wawakilishi wa Tanzania na Ukanda wa CECAFA klabu ya JKT Queens itashuka dimbani kuikabili Mamelodi Sundowns Ladies katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi.

JKT Queens ni kwa mara ya kwanza inashiriki mashindano haya tangu yaanzishwe ikiwa msimu wa kwanza Afrika Mashariki iliwakilishwa na Simba Queens. Mamelodi hii ni mara ya pili kushiriki michuano hii, msimu uliopita walipoteza mchezo wa fainali dhidi ya FAR Rabat.

Kuelekea mchezo huo wa leo Nahodha wa kikosi cha JKT Queens Amina Bilali amesema maandalizi yao ni makubwa ambayo yatatoa ushindani wa kutosha kwa Mamelodi Sundowns hii leo.

Tunafahamu kuwa Mamelodi ni timu kubwa kwa ukanda huu wa Afrika, lakini tumejiandaa kwa ajili ya kuwapa ushindani kama ambavyo makocha wetu wametufundisha.

Nahodha wa JKT Queens, Amina Bilali

Kwa upande wa Mamelodi Sundowns Ladies kupitia kwa nahodha wake Oratile Mokwena mwamejiandaa vizuri kwasababu timu nyingi zinawatazama zaidi wao.

Timu nyingi tunazocheza nazo na hata wale ambao hatuko nao kundi moja wana tutazama sisi, wanatuongezea shinikizo lakini sisi tumejiandaa

Nahodha wa Mamelodi Sundowns, Oratile Mokwena

JKT Quens imepangwa kundi “A” pamoja na Mamelodi Sundowns, CS Casablanca na wenyeji Athletico FC Abidjan.

Mchezo wa ufunguzi utazikutanisha timu mwenyeji mapema hii leo Athletico Abijan dhidi ya CS Casablanca Women kutoka nchini Morocco.

20:00 ATHLETICO FC ABIJAN WOMEN vs SC CASABLANCA WOMEN

IVORY COAST

Makala Nyingine

More in CAF Women Champions League