Connect with us

NBC Premier League

REKODI MECHI 38 ZA SIMBA NA YANGA.

Leo uwanja wa Benjamini Mkapa unaenda kushudia mchezo mkubwa Afrika mashariki na Kati, kati ya Simba na Yanga, hizi ni rekodi za michezo 38 ya mwisho kukutana timu hizi hivi karibuni.

Ligi kuu kandands Tanzania Bara inatarajia kuendelea hii leo kwa mchezo mmoja kupigwa katika dimba la Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam. Mchezo huu utawakutanisha mahasimu wakubwa kwenye soka la Tanzania klabu ya Simba dhidi ya Yanga.

Mchezo huu hujulikana kama mcheze wa watani wa Jadi au Derby ya Kariakoo, Simba itakuwa mwenyeji wa mchezo huu hii leo, Jumapili, November 5.

17:00 SIMBA vs YANGA

UWANJA: Benjamin Mkapa Stadium, Dar Es Salaam.

Hizi ni takwimu za timu zote mbili zilipokutana kuelekea mchezo huu mkubwa nchini Tanzania na Afrika Mashariki na kati.

  • Simba inaingia katika mchezo huu ikiwa mwenyeji wa mchezo mbele ya Yanga.
  • Simba inafundishwa na Mbrazil, Roberto Oliviera na Yanga inafundishwa na Muargentina Miguel Gamondi.
  • Katika michezo 38 ya mwisho ambayo timu hizi zimekutana, Simba imeshinda michezo 11, Yanga imeshinda michezo 11 pia na sare 16 katika mashindano yote.
  • Ligi kuu Kandanda Tanzania Bara hivi karibuni zimekutana mara 32, Simba imeshinda michezo tisa (9), Yanga imeshinda michezo (8) na kutoka sare mara 15.
  • Simba imecheza michezo 16 nyumbani hivi karibuni dhidi ya Yanga. Simba imeshinda michezo sita (6), Yanga imeshinda michezo minne (4) na sare sita (6).
  • Simba imeifunga Yanga magoli 38, na imefungwa magoli 35 katika michezo 38 iliyopita.
  • Mara ya mwisho timu hizi mbili kukutana Simba ilishinda magoli 2-0 ikiwa nyumbani, April 16, 2023.
  • Mara ya mwisho Simba kupoteza mchezo ikiwa mwenyeji wa mchezo dhidi ya Yanga ilikuwa Juni 3, 2021, ilifungwa goli 0-1 na hii ndio ilikuwa mara ya mwisho Yanga kupata ushindi mbele ya Simba.
  • Simba inaingia kwenye mchezo huu ikiwa imecheza michezo sita (6) imekusanya alama zote 18 ikiwa na rekodi ya kutokupoteza mchezo wowote msimu huu ikiwa nafasi ya tatu (3) ya msimamo wa Ligi.
  • Yanga inaingia katika mchezo huu ikiwa imecheza michezo saba (7) ya Ligi, imeshinda michezo sita (6) na imepoteza mchezo mmoja (1) ikiwa nafasi ya pili (2) ya msimamo wa Ligi.
  • Jean Baleke wa Simba na Stephane Aziz Ki wa Yanga ndio vinara wa magoli hadi hivi sasa kila mmoja akifunga magoli sita (6).

Makala Nyingine

More in NBC Premier League