Connect with us

Makala Nyingine

TANZANIA YANG’ARA CECAFA U15.

Timu ya Taifa ya Tanzania U15 imeifunga Somalia katika mchezo wake wa kwanza wa michuano ya CECAFA U15.

Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 15 imeanza vyema mashindano ya CECAFA U15 jana November 5 kwa kushinda mchezo wao wa kwanza dhidi ya timu ya taifa la Somalia kwa goli 1-0.

Goli la timu ya Taifa ya Tanzania lilifungwa na Juma Kaniki Suleiman ambaye aliingia akitokea benchi kwenye dakika 45 za kipindi cha pili.

Juma kaniki ni miongoni mwa hazina za Taifa hili, kwenye michuano ya ligi ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ambayo yalifanyika mwaka huu, Juma alikuwa akiitumika klabu ya Mbeya kwanza, alifanikiwa kufunga magoli 17 na kumaliza nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine