Connect with us

Timu Zaidi

ALIYETIMULIWA NA GARY NEVILLE APATA KAZI.

Kocha wa zamani wa klabu ya Salford City inayomilikiwa na Gwiji wa zamani wa klabu ya Manchester United Gary Neville baada ya kutimuliwa kazi wiki chache zilizopita amepata kazi mpya.

Zikiwa zimepita wiki chache tangu kocha Graham Alexander atimuliwe kazi na klabu ya MK Dons inayoshiriki Ligi daraja la pili nchi England, klabu ya Bradford City imetangaza kuinasa saini yake.

Bradford City imemtangaza kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 jana Jumatatu, November 6 ambaye atatumika klabu hapo hadi mwaka 2025. Chris Lucketti ataungana na Alexander kwenye kikosi hicho kama kocha msaidizi.

Ni furaha kuwa hapa, nina furaha ya majukumu, umuhimu wa timu na klabu. Mimi na Chris tumekuwa tukija hapa mara chache kucheza dhidi ya Bradford City, lakini itakua vyema sasa kuwa mahali sahihi kwasasa.

Uwanja ukiwa umejaa na mashabiki wanaipa nguvu timu yao, huwa ni uwanja mgumu sana kuja kucheza hapa, tunatakiwa kuifanya iwe sehemu ngumu zaidi kwa yoyote atakayekuja hapa.

Ukijiunga na klabu, unatakiwa kutazama maboresho ya muda mfupi ambayo unaweza kuyafanya na pia kutazama umuhimu wa kile utakachokifanya. Kwangu mimi hilo halina mwisho.

Ninashauku sana mwisho wa wiki hii, hautaniona nimekaa sana, lakini tunajua namna ambavyo huu uwanja unavyokuwa wakati wa mchezo, na tunatazamia mashabiki zetu kuwapa furaha.

Alexander Akizungumza baada ya kutambulishwa.

Alexander amejiunga na Bradford baada ya kipindi kifupi tangu kuachana na klabu ya MK Dons, ambaye pia aliiongoza klabu hiyo kwenye michezo kumi na sita (16) pekee, akishinda michezo sita (6). sare nne (4) na amepoteza michezo sita (6).

Alexander amewahi kuzifundisha klabu za Motherwell, Scunthorpe, Fleetwood na pia aliwahi kupita Salford City inayo milikiwa na Nicky Butt, Ryan Giggs, Paul Scholes na Neville brothers ambapo aliiongoza timu hiyo kucheza michezo 105 kabla ya kuondoshwa klabuni hapo.

Alitimuliwa Salford October 2020 na nafasi yake kuchukuliwa na Paul Scholes, lakini baadae Gary Neville alikiri kwa kusema kuwa maamuzi ya kumfukuza kocha huyo yalifanyika kimakosa.

Graham Alexander hakutakiwa kuondoka kwenye hii klabu msimu uliopita, sikutakiwa kufanya ule uamuzi nilioufanya.

Alisema Gary Neville.

Alexander kabla ya kugeuka kuwa kocha alikuwa mchezaji kwa takribani miaka 24 na alipita katika klabu mbalimbali ikiwemo Scunthorpe United, Luton Town na Burnley zote za nchini England, ametumia muda mwingi wa soka kucheza katika klabu ya Presto North End na amecheza timu ya Taifa ya Scotland michezo 40.

Makala Nyingine

More in Timu Zaidi