Kamati ya mashindano ya CHAN ipo kwenye mazungumzo ya kurekebisha sheria kuhusu wachezaji wanaotakiwa kutumika kwenye mashindano hayo. mashindano hayo yalikuwa yakiwahusisha wachezaji wanaocheza kwenye Ligi zao za ndani. Kikao cha kamati kinaongozwa na Rais wa CAF, Patrice Motsepe.
Tutalizungumza hili kwenye kamati kuu, huu utakuwa na mwanzo wa mapinduzi ya soka la ndani CHAN. Kitu cha msingi ni kwamba wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika watambulike na wacheze michuano hii.
Unaweza kuwa mchezaji wa Algeria unayecheza kwenye klabu iliyopo Misri na ukaliwakilisha Taifa lako kwenye michuano ya CHAN.
Kenya watakuwa wenyeji wa mashindano hayo mwaka 2024.
Alisema Patrice Motsepe, Rais wa CAF.