16:00 Simba vs Namungo
Uwanja: Uhuru
Ligi kuu kandanda Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea hii leo kwa mchezo mmoja katika dimba la Uhuru Jijini Dar Es Salaam ambapo klabu ya Simba itaikaribisha Namungo. Hizi ni rekodi za timu hizi mbili kuelekea mchezo huu.
- Simba inaingia katika mchezo huu ikiwa nafasi ya tatu (3) ya msimamo wa Ligi, ikicheza michezo saba (7), imeshinda michezo sita (6), imepoteza mchezo mmoja (1), imefunga magoli 17 imefungwa magoli 10 ikiwa na alama 18.
- Namungo ipo nafasi ya 12 ya mimamo wa Ligi, ikicheza michezo nane (8), imeshinda mchezo mmoja (1), sare nne (4) na imepoteza michezo mitatu (3), imefunga magoli saba (7) na imefungwa magoli nane (8), ikiwa na point saba (7).
- Timu hizi mbili zimekutana mara tisa (9) kwenye mashindano yote, Simba ikishinda mara sita (6) na kutoka sare mara tatu (3), Namungo haijawahi kupata ushindi.
- Ligi kuu Tanzania Bara timu hizi zimekutana mara nane (8), Simba imeshinda mara tano (5), sare tatu (3), Namungo haijawahi kupata ushindi.
- Simba imeifunga Namungo magoli 17, Namungo imeifunga Simba magoli saba (7).
- Simba imecheza michezo minne ikiwa nyumbani na haijawahi kupoteza mchezo wowote. Mara ya mwisho Simba ilishinda 1-0 ikiwa nyumbani dhidi ya Namungo.
Kocha wa Namungo Dennis Kitambi kuelekea mchezo huu amesema watapita katika mbinu ambazo walitumia Al Ahly na Yanga kuisumbua Simba katika mchezo wa leo.
Tunaenda kucheza na Simba, ila mechi tatu zilizopita zimetupa mwanga wa namna ya kucheza nao kwa maana ameruhusu goli kila mechi, kwakuwa tunafahamu hilo sisi tutaingia kuwashambulia kwakuwa tunajua lazima tutapata goli.
Dennis Kitambi kocha wa Namungo.
Sisi Namungo ni kama Fisi, ni mwendo wa kukusanya mizoga aliyoiacha Yanga, walimfunga Azam na sisi tukamfunga, wamemfunga Simba na sisi kama kawaida tunaenda kuokota mzoga leo.
Kelvin Sabato, mchezaji wa Namungo kuelekea mchezo wa leo.
Simba itaingia katika mchezo huu ikiwa chini ya kocha wa magolikipa Daniel Cadena ambaye anakaimu nafasi ya kocha mkuu baada ya aliyekuwa kocha mkuu Roberto Oliviera kufungashiwa vilago amesema wamejiandaa vizuri na wanategemea mchezo mgumu kutoka kwaa Namungo.
Tumewaandaa vizuri wachezaji kwaajili ya mchezo wa leo dhidi ya Namungo. Tunawaheshimu wapinzani, na tumewafuatilia, tunategemea kupata mchezo mgumu lakini tumejipanga kupata matokeo.
Daniel Cadena, Kaimu Kocha mkuu Simba.
Wachezaji wote maandalizi yetu ni mazuri kuelekea kwenye huu mchezo kuhakikisha tunapata alama tatu. Tumejiandaa kulingana na aina ya mpinzani ambaye tutakutana naye ili kupata ushindi. Hatuangalii kilichopita tunaenda kukutana na mpinzani mgumu ila tutapambana na kupata matokeo mazuri dhidi yao.
John Bocco, Nahodha wa kikosi cha Simba kuelekea mchezo dhidi ya Namungo leo.