Manchester United jana Jumatano imepokea kichapo cha nne kwenye Ligi ya mabingwa Barani Ulaya kutoka kwa Copenhagen cha 4-3, kipigo hicho kimeifanya Manchester Unite iwe mkiani mwa msimamo wa kundi hilo. Ikimaliza hivi itaondoshwa kabla ya hatua ya mtoano.
Vijana wa Erik Ten Hag wanaendelea kuhangaika kwenye Ligi kuu kandanda England wakipoteza michezo mitano (5) katika michezo 11 ya kwanza ya Ligi hiyo. Manchester United ipo nafasi ya nane ya msimamo wa Ligi kuu.
Mchezo wa mwisho kabla ya kupisha mechi za timu za Taifa kwa Manchester United utakuwa dhidi ya Luton wakiwa nyumbani Old Trafford Jumamosi hii. Huenda Ten Hag akatimuliwa kikosini hapo mwezi ujao kama matokeo hayatakuwa mazuri kwa upande wake.
Kama Manchester United itakubali kupoteza mchezo dhidi ya Liverpool mchezo ambao utapigwa Jumapili, December 17, Jumatatu ya December 18 Asubuhi huenda akatimuliwa, tarehe hiyo itakuwa sawa na ile aliyotimuliwa kocha wa zamani wa klabu hiyo Jose Morinho miaka mitano iliyopita.
Mashabiki tayari wameshaanza kupiga kelele kuhusu kuondoshwa kwa Erik Ten Hag kama akipoteza mchezo wake dhidi ya Liverpool. Mmoja alisema;
Manchester United hawatamfukuza Ten Hag kesho, watamfukuza baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Liverpool kabla ya Christmas. Hivyo ndivyo watakavyofanya.
Shabiki mmoja wa klabu alisema,
Natumaini Ten Hag hatafukuzwa kabla ya mchezo dhidi ya Liverpool.
Shabiki mwingine alizungumza.
Ndugu zangu bodi ya Manchester United na mashabiki , Ten Hag alindwe kwa namna yoyote ile hadi December 17.
Huyu pengine alikuwa shabiki wa Liverpool.
Ten Hag ni kocha wa tano kuifundisha Manchester United tangu alipoondoka Sir Alex Ferguson miaka kumi (10) iliyopita.
David Moyes, Louis van Gaal, Mourinho na Ole Gunnar Solskjaer wote walifeli kubeba kombe la Ligi kuu nchini England tangu 2013.