Connect with us

Chan

WINFRIDA HAZINA KUBWA KWA TWIGA STARS.

Moja kati ya washabuliaji hatari zaidi kwasasa kwenye soka la wanawake asiyeogopa kufika na mwenye uwezo mkubwa wa kupiga chenga.

Nyota wa klabu ya JKT Queens na timu ya Taifa ya Tanzania ya wanawake (Twiga Queens) Winfrida Gerald ni miongoni mwa nyota walio kwenye kiwango bora zaidi kwasasa.

Winfrida aliibuka mfungaji bora akiwa na Fountain Gate Princess katika mashindano ya shule yaliyofanyika nchini Afrika Kusini mapema mwaka huu.

Tangu hapo Winfrida amekuwa akipata nafasi mara kwa mara ya kucheza katika timu za Taifa za Tanzania kwa ngazi zote na kiwango chake kinazidi kuimarika kila kukicha.

Jana JKT Queens ilikuwa na kibarua kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa Barani Afrika dhidi ya Athletico d’Abidjan, mchezo ambao ulikuwa mhimu zaidi kwa JKT Queens maana kama wangepoteza walikuwa wanaondolewa rasmi kwenye mashindano.

Winfrida aliingia akitokea bencho dakika ya 46 baada ya kipindi cha pili kuanza wakati ambao JKT Queens ilikuwa nyuma kwa goli 1-0.

Winfrida aliisumbua sana safu ya ushambuliaji ya Athletico na dakika ya 66 ya mchezo akaiandikia goli bora kwelilweli timu yake, hakuishia hapo aliendelea kulisakama lango la Athletico hadi walipopata goli la kuongoza dakika ya 88 ya mchezo.

Moja kati ya washabuliaji hatari zaidi kwasasa kwenye soka la wanawake asiyeogopa kufika na mwenye uwezo mkubwa wa kupiga chenga.

Mechi inayofuata ya JKT Tanzania waliopo katika nafasi ya pili ya msimamo wa kundi A ni dhidi ya Clab Sporting Casablanca ya Morocco.

Kila lakheri wawakilishi wa Taifa kwenye mashinda makubwa Barani Afrika.

Makala Nyingine

More in Chan