Golikipa wa zamani wa klabu ya Manchester United David De Gea yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Real Betis ya nchini Hispania kwaajili ya kujiunga na kikosi hicho mwezi January kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Hispania.
De Gea amekuwa hana timu kwa takribani miezi minne sasa tangu alipoachana na klabu yake ya zamani ya Manchester United kwenye dirisha kubwa la usajili la majira ya kiangazi.
Real Betis ili ikamilishe usajili wa David De Gea ni lazima imuondoshe mchezaji mmoja kwenye kikosi chao ili ikwepe matumizi makubwa ya pesa za usajili. Hata hivyo De Gea atajiunga na kikosi hicho mwezi January kama wakikubaliana na klabu hiyo.
Mlinzi wa klabu hiyo Rui Silva anatajwa kuondoka kikosini hapo ili kuupisha usajili wa golikipa huyo wa Hispania.
Vijana wa Manuel Pellegrini kwasasa wapo nafasi ya sita ya msimamo wa ligi kuu nchini Hispania na wapo kileleni mwa msimamo wa kundi kwenye michuano ya Europa.
David De Gea miezi kadhaa iliyopita alihusishwa na tetesi za kurejea kwenye klabu ya Manchester United mwezi January kwaajili ya kuziba nafasi ya Andre Onana atakayeondoka klabuni hapo kwaajili ya michuano ya AFCON 2023.