Connect with us

African Football League

SIMBA YASHINDA TUZO YA MASHABIKI BORA.

Klabu ya Simba imeshinda tuzo ya Mashabiki bora wa michuano ya African Football League 2023 yaliyomalizika hii leo nchini Afrika Kusini. Tuzo hiyo imepokelewa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo Salim Abdallah ‘Try Again’.

Simba imebeba tuzo hii baada ya mashabiki wake kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hii uliofanyika nchini Tanzania katika uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam kati ya timu yao ya Simba na klabu ya Al Ahly [Misri] mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana goli 2-2.

Baada ya Mashabiki wa Simba kutangazwa kuwa mashabiki bora wa AFL 2023, Afisa habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally ameandika katika ukurasa wake wa instagram kuwa Simba ina wanachama na sio wanywa supu kwa kuwakashfu watani wao wa jadi Yanga ambao walikuwa na zoezi la kunywa supu hii leo.

Tumeshinda tuzo ya mashabiki bora wa Africa. Hongereni sana wana Simba mnastahili heshima hii, mmeonesha tofauti ya mashabiki wa mpira na wanywa Supu za vibudu.

Sifa hiii ya Ubora tunapaswa kuilinda na kujivunia maana sio kila mtu anaweza bora. Kuilinda sifa hii ya ubora ni pamoja na kuwa wavumilivu pindi timu inapopitia nyakati ngumu.

Ahmed Ally ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mabingwa wa jumla wa michuano hii ni Mamelodi sundowns waliotwaa taji la kwanza la African Football League 2023 kwa kumfunga Wydad AC kwa jumla ya magoli 3-2 baada ya michezo yote miwili na katika mchezo wa leo wakiwa nyumbani wameshinda goli 2-0, katika mchezo wa kwanza walikubali kichapo cha 2-1.

TUZO ZINGINE

Mchezaji Bora wa mashindano – Thapelo Maseko [ Mamelodi Sundowns]

Mfungaji bora wa mashindano – Thapelo Maseko [Mamelodi Sundowns]

Golikipa bora wa mashinano – Ronwen Williams [Mamelodi Sundowns]

Bingwa wa mashindano – Mamelodi Sundowns.

Makala Nyingine

More in African Football League