Connect with us

African Football League

WYDAD AC HAIJAWAHI KUSHINDA AFRIKA KUSINI.

Michuano mipya ya African Football League inatarajiwa kutamatika hii leo kwa mchezo wa pili wa fainali kuchezwa katika uwanja wa Loftus Versfield uliopo Pretoria nchini Afrika Kusini. Mamelodi Sundowns ikiwa nyumbani wataikabili Wydad AC.

Mchezo wa kwanza wa timu hizi mbili ulipigwa nchini Morocco katika uwanja wa Mohamed V uliopo katika mji wa Casablanca, ulimalizika kwa mwenyeji Wydad AC kuibuka na ushindi wa goli 2-1. Ushindi huo bado hauwapi faida kubwa kuelekea katika mchezo wa hii leo.

Timu hizi katika michezo 13 iliyopita, Mamelodi Sundowns imeshinda mechi tatu (3), imetoa sare mechi tano (5) na imepoteza mechi tano (5). Katika uwanja wa Loftus Versfield timu hizi zimekutana mara sita (6), Mamelodi Sundowns ikishinda michezo mara tatu (3) huku ikitoa sare tatu (3). Wydad AC haijawahi kupata ushindi tangu mwaka 2017.

Katika michezo sita (6) ya mwisho Mamelodi Sundowns imeshinda mchezo mmoja pekee sare nne (4) na Wydad AC imeshinda mchezo mmoja (1)

Mchezo wa mwisho kupigwa katika dimba la Loftus Versfield timu hizi zilitoshana nguvu ya kufungana goli 2-2. Hadi kufika fainali Mamelodi Sundowns imeitoa Petro Atletico ya Angola na Al Ahly ya Misri, huku Wydad AC ikiitoa Enyimba ya Nigeria na Esperance de Tunis ya Tunisia.

Shamla shamla za fainali hizi zitapambwa na wasanii kadhaa watakaotumbuiza mbele ya umati wa watu watakaojitokeza hii leo akiwemo Daliwonga,DJ Maphorisa, Young Stunna, Cassper Nyovest na Makhadzi.

Makala Nyingine

More in African Football League