Connect with us

EPL

MAGUIRE ANA FURAHA MAN UNITED.

Beki wa Manchester United Harry Maguire ana furaha kusalia katika kikosi hicho na kupigania nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha Erik ten Hag.

Licha ya kuripotiwa ofa kutoka kwa West Ham kujiunga nao msimu wa joto, Maguire aliamua kusalia tena United na beki huyo sasa anahisi kuwa amethibitishwa kwa uamuzi wake huo baada ya kuanza katika mechi nane zilizopita za Mashetani Wekundu kwenye michuano yote.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, amekuwa mtu asiyekuwa na furaha tangu Ten Hag ajiunge na klabu hiyo msimu uliopita, akiwa amecheza mechi 16 za Premier League na kutumia dakika 759 pekee uwanjani. Hata hivyo mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza hakukata tamaa. Tangu Lisandro Martinez awe nje ya uwanja mwishoni mwa Septemba sababu ya majeraha, Maguire amekuwa mhimili mkuu wa timu ya klabu hiyo na alidai kuwa anafurahia soka lake kwa sasa.

Nilicheza michezo michache mwaka jana, 16 au 17 nilianza, na nilihisi kama nilifanya vyema katika michezo niliyocheza, sikucheza nyingi kama ambavyo nilikuwa napenda. Kwa upande mwingine, Rapha [Raphael Varane] na Licha [Lisandro Martinez] walikuwa wakicheza kwa ustadi mkubwa.

Akizungumza Harry Mguire wakati akifanya mahojiano na ESPN

Ilibidi nitumie wakati wangu na kuwa mvumilivu. Nilikuwa na nafasi mbili au tatu msimu uliopita za kupata mfululizo wa michezo lakini niliugua, niliugua majeraha mara mbili, kwa hivyo sikupata muda wa kucheza mechi ambazo niliamini ningeweza kudhihirisha ubora wangu kwa kocha. Nimepata hivyo sasa. Ninafurahia sana soka langu na ninafurahia sana kuichezea klabu hii. Nilikuwa tayari kubaki na kupigania nafasi yangu na tuna mabeki wa kati wanne au watano wa juu wa kimataifa katika klabu hii na ushindani wa nafasi ni mkubwa sana.

Kufanya kazi kwa bidii katika kiwanja cha mazoezi ni jambo la muhimu na kuhakikisha kuwa uko tayari. Nilianza michezo 16 au 17 mwaka jana na nilihisi kama kiwango changu kilikuwa vizuri. Kulikuwa na mazungumzo mengi kunihusu kwa sababu sikuwa nikicheza michezo mingi, lakini ndivyo ilivyo. Nilikuwa nikiichezea nchi yangu vizuri, nilikwenda Kombe la Dunia na kucheza vizuri na siku zote nilifikiri kiwango changu kilikuwa vizuri. Lakini ninachuana na mabeki wa kati wa kiwango cha juu na mwaka jana walikuwa wakicheza kwa kustaajabisha, kwa hivyo sikupata nafasi nyingi. Klabu hii inadai ushindani wa nafasi na ndivyo tulivyo katika nafasi yangu.

Aliongeza Harry Maguire.

Makala Nyingine

More in EPL