Connect with us

Simba

SVEN KUIKACHA SIMBA KUTUA AFRIKA KUSINI.

Kocha wa zamani wa Wydad Athletic Club Sven Vandenbroeck amekiri kuwa anavutiwa zaidi kufanya kazi kwenye Ligi kuu nchini Afrika Kusini licha ya kuhusishwa kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Simba inayoshiriki Ligi kuu Tanzania Bara.

Navutiwa na zote, kuifundisha Simba au klabu yoyote inayoshiriki Ligi kuu Afrika Kusini.

Naijua klabu na mazingira yake. Wana mashabiki wazuri na wapenda mpira pia. Simba ina faida ya Ligi ya mabingwa lakini kwenye Ligi ya ndani ina mechi za ugenini ambazo ni mbaya kwao wanaweza kupoteza.

Ligi ya Afrika Kusini ina thamani kubwa na miundimbinu yake kwa ujumla ni mizuri sana.

Sven akizungumzia kuhusu kuhusishwa kwake kujiunga na Simba na Ligi kuu Afrika Kusini.

Kuhusu kudumu kwenye klabu za CR Belouzdad na Wydad AC kwa muda mfupi Sven amesema,

Naweza kutoa jibu fupi kwa swali hili [Kwanini sikukaa kwa muda mrefu na miamba ya Kaskazini mwa Afrika].

Pale Wydad nilikuwa kocha wa tano (5) kwenye msimu ule. Nilisaini mkataba wa miezi minne (4) ukiwa na chaguo la mwaka mmoja, ili niongeze huo mwaka ilibidi nibebe ubingwa wa Ligi ya mabingwa Afrika na unajua tulipoteza fainali dhidi ya Al Ahly.

CR Belouzdad ni stori nyingine. Rais alikuwa anapanga kikosi chake na kuanza kunishinikiza kianze kikosi kama alivyopanga yeye.

Lakini pia usajili wa wachezaji wawili wa kimataifa wenye umri wa miaka 36 uliofanywa siku ya mwisho ya usajili kulizua gumzo sana.

Klabu ilikuwa inataka wote wacheze na nilikuwa naona bado hawapo tayari kuanza kutumika.

Kuna mchezo sikumuanzisha kwenye kikosi mmoja wao, Rais aliweka wazi mbele ya vyombo vya habari kuwa mchezaji alikuwa anaumwa na mimi niliwaambia waandishi wa habari kuwa hakuwa sehemu ya mipango na matumizi yangu.

Baada ya hapo, niliamua kuachana na klabu hiyo kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Sven Vandenbroeck akizungumza kuhusu kutokudumu kwa muda mrefu nchini Morocco na Algeria.

Makala Nyingine

More in Simba