Connect with us

Makala Nyingine

TANZANIA YAONDOSHWA CECAFA, ZANZIBAR KUIFUATA UGANDA FAINALI?

Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 15, imeondoshwa kwenye mashindano ya CECAFA U15 hatua ya nusu fainali baada ya kukubali kichapo cha 2-1 kutoka kwa Uganda Rhinos(Uganda U15), mchezo uliopigwa kwenye Kituo cha Ufundi ca FUFA, jijini Njeru, Uganda.

Wenyeji walitangulia kupata bao la kuongoza dakika ya 12 kupitia kwa Nahodha Abubakar Walusimbi, kabla ya mlinzi, Samuel Mubiru kufunga bao la pili dakika chache kabla ya kwenda mapumziko akiunganisha kwa kichwa mpira wa pigo la kona.

Tanzania walipata goli la kufutia machozi dakika ya 83 ya mchezo kupitia kwa Feisal Juma, hata hivyo Uganda walishikilia uongozi wao mpaka dakika ya 90 kumalizika na kufanikiwa kutinga hatua ya Fainali ya michuano hii.

Uganda Rhinos wanasubiri mshindi kati ya Sudani ya Kusini dhidi ya Zanzibar kummpata mpinzani wao kwenye fainali itayochezwa Alhamisi ya wiki hii, tarehe 16/11/2023 huko huko nchini Uganda.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine