Connect with us

NBA

BADO NIKO FITI – LEBRON JAMES

Mchezaji wa Los Angeles Lakers wa ligi ya kikapu ya nchini marekani na Staa wa mchezo huo nchini humo, LeBron James, 38 amesema kuwa bado anahisi vile vile kama alivyokuwa kwenye miaka yake ya 20 na kitu kwenye uwanja wa kuchezea.

Bado najihisi vile vile tu kama nilivyokuwa kwenye miaka yangu ya Ujana(20s) nikiwa uwanjani. Naingia tu wanjani kama kawaida na kuwa pale kwa ajii ya wenzangu na kuisaidia timu. Sioni kama kuna ambacho nashindwa kufanya. Bado naweza kukimbia, kufungia mbali(3s), kufunga karibu, kupiga pasi za usaidizi, kugombea mipira. Hivyo bado niko fiti.

James, Mzaliwa wa Akron, Ohio, anaingia msimu wake wa 21 sasa tangu aanze kucheza NBA mwaka 2003 akiwa na Clevelend Cavaliers. Alicheza kwa misimu 7 kabla ya kujiunga na Miami Heat 2010. Mwaka 2014 baada ya miaka 4 tangu kuondoka Cleveland, alirejea kwenye timu yake na kuipa ubingwa wa NBA kabla ya 2018 kuhamia LA Lakers mpaka hivi leo.

 LeBron James alirejea kikosini jana na kuingoza Lakers kupata ushindi wake wa 6 msimu huu wakiwafunga Memphis Grizzlies vikapu 134-107. Shoo ilisimamiwa vema na vijana D’angelo Russel aliyefunga vikapu 24, kurejesha mipira 3 na pasi za usaidizi 5. Rui Hachimura akifunga vikapu 23 na Antony Davis akifunga vikapu 19 kupeleka msiba huo kwa Grizzlies.

Makala Nyingine

More in NBA