Israel ametoka kupoteza kwenye mchezo wake dhidi ya Kosovo kwenye mechi yake ya 7 ya kundi Ikwa bao 1-0 na leo wanacheza mchezo wao wa 8 dhidi ya timu ngumu ya Uswisi.
Switzerlanda wana alama 15 wakiwa nafasi ya 2 na wanafahamu umuhimu wa kushinda mchezo wa leo ili Israel yenye alama 11 wasimmsogelee. Wakiwa wameshinda mechi 2, sare 3 wanajua haitakuwa rahisis dhidi ya Israel waliojeruhiwa ambao walionyesha mchezo mzuri dhidi ya Kosovo licha ya kupoteza lakini uimara wa Switzerlanda kuna asilimia kubwa wakaibuka na ushindi.
DONDOO: SWITZERLAND USHINDI
Rwanda walicheza dhidi ya wababe Senegal kwenye mchezo wao wa mwisho wa kufuzu AFCON ulioisha kwa sare ya 1-1, lakini kiuhalisia, Senegal walikuwa washafuzu. Rwanda hawakuwa wazuri kihivyo na hata kampeni yao ya kufuzu ilikua sio nzuri.
Wakiwategemea zaidi, Olivier Niyonzima, Muhadjiri Hakizimana na Yves Kimenyi, wanakutana na Zimbabwe yenye mipango mizuri ya kisoka hivi sasa kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi C wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026. Walitoka sare ya 1-1 kwenye mchezo kirafiki dhidi ya Botswana. Ni uhalisia kuwa mchezo huu hautokuwa na ukwasi wa magoli.
DONDOO : MAGOLI CHINI YA 3.5
Gael Kakuta, Cedric Bakambu na Arthur Masuaku, walipeleka kilio kwa Mauritania cha 3-1(goli la Aly Abeid), mara ya mwisho timu hizi mbili kukutana kwenye kuwania kufuzu AFCON kundi I. Hata hivyo timu zote hizi zikafanikiwa kufuzu kucheza AFCON 2023 Ivory Coast. Bila shaka ni Mechi ngumu kummtabiri mshindi.
Simba wa Chinguetti, Mauritania wameshinda mechi zao 3 za mwisho, 2-1 dhidi ya Madagascar, 2-1 dhidi ya Gabon na 3-0 dhidi ya Sudan. Hawana tabu kwenye kupata magoli lakini pia wanaruhusu. Na kucheza dhidi ya washambuliaji wenye njaa kama Fiston Mayele, Meshack Elia, Makabi Lilepo, Jackson Muleka, Dieumercie Mbokani, Jonathan Bolingi na Theo Bongonda pamoja na Cedric Bakambu, hutarajii hii mechi kuisha bila magoli zaidi ya 2.5 au GG
DONDOO : TIMU ZOTE KUFUNGANA AU MAGOLI ZAIDI YA 2.5