Connect with us

NBA

BOSTON CELTICS WAZIDI KUPASUA NBA

Boston Celtics, usiku wa kuamkia leo walifisha ushindi wao wa 9 msimu huu huku wakipoteza 2 tu kwenye michezo yao 11 baada ya kuwanyuka timu nyingine ngumu msimu huu Philadelphia 76ers vikapu 117-107, ambao sasa wanapoteza mchezo wao wa pili mfululizo baada ya kufungwa na Indiana Pacers mchezo uliopita wa In-Season.

Jayson Tatum na Derrick White walikuwa vinara wa vikapu wakifunga jumla ya vikapu 56(Tatum-29, White-27) huku Jrue Holiday(18) na Al Horford(14) wakifuatia kwenye kuisulubu 76ers kwenye mchezo ambao ulikuwa na ushindani wa aina yake hasa kwa namna Joel Embiid alivyokuwa akiiongoza timu yake kupambana licha ya kupoteza.

Matokeo Mengine:

Lakers  walipoteza kwa vikapu 125-110 dhidi ya Orlando Magic. Portland Trail Blazers wakinyukwa nyumbani 95-109 na Cleveland Cavaliers. Viakpu 31 vya Kevin Durant vilichangia timu yake ya Phoenix Suns kuwachapa Minnesota Timberwolves 133-115 wakati Alex Carruso na wenzake walishindwa kuihimili nguvu kazi ya Orlando Magic, Bulls 94-96 Orlando.

Kwingineko, Atlanta Hawks walifungwa vikapu 116-114 na New York Knicks na Giannis Antentokounmpo aliendelea kuitakatisha Milwaukee Bucks, wakishinda kwa vikapu 128 dhidi ya 112 vya Toronto Raptors.

Mechi zengine zitaendelea usiku huu wa kuamkia kesho zikiwakutanisha Miami Heat v Brooklyn Nets na Golden State Warriors dhidi ya Oklahoma City Thunder. Game zote za Moto

Makala Nyingine

More in NBA