Connect with us

AFCON

FRANK: TIMU ZINGINE ZINAIOGOPA NIGERIA AFCON 2023.

Kiungo wa timu ya Taifa ya Nigeria na klabu ya Brentford Frank Onyeka anaamini nchi zingine zinaihofia Nigeria kutokana na mkusanyiko wa vipaji vingi kwenye kikosi chao, huku akiamini wanaenda kutwaa ubingwa mwingine wa AFCON tangu mwaka 2013.

Nigeria ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi ya kufanya vizuri katika michuano hii inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi January 9, 2024, kutokana na kuwepo wachezaji wengi nyota wanaofanya vizuri Barani Ulaya.

Victor Osimhen anatajwa kuwa mshambuliaji bora kwasasa Barani Ulaya, huku Victor Boniface akifanya vizuri Ujerumani na Taiwo Awoniyi akifanya mabalaa nchini England.

Onyeka mwenye umri wa miaka 25 anatarajiwa kuiongoza timu hiyo katika michezo ya kufuzu fainali ya kombe la Dunia 2026 dhidi ya Zimbabwe na Lesotho na mchezo wa ufunguzi wa AFCON dhidi ya Equatorial Guinea January 14, 2024.

Kuelekea michezo hii miwili ya kutafuta tiketi za kufuzu fainali za kombe la Dunia 2026, kiungo huyo wa Brentford amesema;

Nafikiri tuna timu nzuri ambayo inaweza kwenda na kupata matokeo. Timu nyingi zinaiogopa sana Nigeria. Nasema hivyo kwasababu ya aina ya kikosi tulichonacho, tunaweza kwenda na kushinda.

Una Victor Osimhen, Victor Boniface, Taiwo Awoniyi ambao wote wanafanya vizuri Barani Ulaya. Tuna timu nzuri ambayo tutaenda kushinda na kubeba kombe.

Tuna wachezaji wengi wa zamani waliofanya vizuri wakiwa na Nigeria lakini kwasasa ni kwetu sisi wachezaji, tunahitaji kuzingatia wenyewe kama timu kufanya ambacho tunahitaji kufanya ili Taifa lijivunie.

Frank Onyeka akieleza.

Victor Osimhen na Taiwo Awoniyi ni miongoni mwa washambuliaji wanaofanya vyema kwa sasa ambao wanatazamwa zaidi kuelekea katika fainali hizi kubwa Barani Afrika.

Licha ya kuwa na wachezaji nyota wengi kwenye kikosi timu ya Taifa ya Nigeria ilishindwa kufuzu fainali hizo mwaka 2015 na 2017 lakini hata waliposhiriki fainali hizo mwaka 2021 waliondoshwa hatua ya 16 bora.

Hicho ndicho kinaongeza presha kwa kikosi cha sasa cha Super Eagle kuelekea michuano ya mwaka huu inayofanyika January, 2024 nchini Ivory Coast.

Tuna presha kwasababu Nigeria ni kubwa, ina idadi kubwa ya watu takribani million 200. Kwahiyo kila mchezo, kila mashindano, wanatarajia sisi tushinde, siku zote tunakuwa na shinikizo kubwa.

Lakini ni vizuri kwasababu, utaona nchi yote wanaangalua mpira na wanataka sisi tufanye. Kwahiyo hicho ni kitu kizuri kwetu na kinatupa nguvu ya kufanya vizuri.

Frank Onyeka aliongeza.

Onyeka anajulikana kama Frank the Tank, alifunga goli lake la kwanza wakati wa mapumziko ya michezo ya kimataifa yaliyopita wakati Nigeria ikishinda goli 3-2 dhidi ya Msumbiji.

Anaeleza namna ambavyo ilikuwa baada ya kufunga goli lake la kwanza akiwa na uzi wa Nigeria.

Ilikua maalumu, nilikuwa nahofia nafasi kama hiyo hakitatokea lakini ninafuraraha nilifunga. Nilifunga goli na tulipata ushindi, kwahiyo nilikuwa na furaha sana. Najivunia na najua familia yangu ilikuwa inajivunia pia.

Ni kitu kikubwa kama mchezaji wa Nigeria, kupata goli lako la kwanza kwaajili ya timu yako ya Taifa, kwahiyo nina furaha sana kuhusu goli lile.

Onyeka alieleza hisia alizozipata baada ya kufunga goli lake la kwanza akiwa na timu ya Taifa.

Safari ya Frank Onyeka hadi kuwa mchezaji tegemezi ndani ya Brentford inayoshiriki Ligi kuu soka England na timu ya Taifa ya Nigeria ilianzia kwenye mitaa ya Benin City akiwa mchezaji mdogo kabisa.

Hadi hivi sasa amecheza michezo 14 ya kimataifa na anaendelea kuamini kuwa watafanya vizuri zaidi.

Kila mchezaji nyumbani ana ndoto za kucheza kwenye kiwango kikubwa kwenye Ligi kubwa kama ya England. Nilipokuwa nakua, Nilikuwa najiamini mwenyewe kuwa nitakua naichezea timu yangu ya Taifa, kuiwakilisha kwenye mashindano.

Yalikuwa malengo yangu kucheza kwenye Ligi kubwa na huwezi jua kama utafika huko. Lakini nina furaha nimefanikiwa kwa haraka zaidi.

Frank Onyeka.

Makala Nyingine

More in AFCON