Connect with us

NBC Championship

AUCHO APIGWA RUNGU, TFF KUKUSANYA MILLION 16.

Bodi ya Ligi kuu kandanda Tanzania Bara imemtia hatiani kiungo wa klabu ya Young Africans Khalid Aucho kutokana na kumfanyia madhambi ya makusudi [kumpiga kiwiko] nyota wa klabu ya Coastal Union ya Tanga, Ibrahim Ajibu katika mchezo wa Ligi kuu uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0 mchezo uliochezwa katika dimba la Mkwakwani, Tanga.

Aucho amefungiwa kucheza michezo mitatu (3) ya Ligi kuu na kombe la shirikisho sambamba na faini ya laki tano (500,000).

Kwenye mchezo huo pia klabu ya Coastal Union imetozwa faini ya million oja [1,000,000] kwa kosa la wachezaji wake kuchelewa kutoka nje ya chumba cha kuvalia nguo, jambo lililosababisha mchezo huo kuchelewa kuanza.

Lakini pia mwamuzi wa mchezo huo Emmanuel Mwandembwa [Arusha] amefungiwa miezi sita kuchezesha kwa kushindwa kumudu mchezo huo.

MECHI NAMBA 56: SIMBA 2-1 IHEFU.

Mashabiki wa Simba walioonekana kumpiga shabiki aliyekuwa amevalia jezi ya Yanga wamefungiwa kuingia uwanjani kwa miezi Sita.

MECHI NAMBA 45: SIMBA 1-5 YANGA

Yanga imetozwa faini ya Million tano [5,000,000] kwa kosa la kuingia uwanjani kupitia mlango usio rasmi.

Simba imtozwa faini ya Million Moja [1,000,000] kwa kosa la wachezaji wake kuchelewa kutoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, jambo lililosababisha kuchelewa kuanza kwa mchezo.

Mchezaji wa Simba Kibu Dennis ametozwa faini ya Laki tano [500,000] kwa kosa la kushangilia mbele ya mashabiki wa Yanga baada ya kufunga goli pekee kwa Simba.

Mchezaji wa Simba Henock Inonga Baka ametozwa faini ya laki tano [500,000] kwa kosa la kushangilia mbele ya benchi la ufundi la Yanga.

Kocha msaidizi wa Yanga, Moussa Ndao ametozwa faini ya laki tano [500,000] kwa kosa la kuwatolea lugha ya matusi maafisa wa Simba.

Golikipa wa Yanga, Djigui Diarra ametozwa faini ya laki tano [500,000] kwa kosa la kushangilia goli mbele ya benchi la ufundi la Simba

MECHI NAMBA 65: KMC 1-2 DODOMA JIJI FC

KMC imetozwa faini ya Million moja [1,000,000] kwa kosa la kuchelewa kufika uwanjani.

MECHI NAMBA 69: MASHUJAA 1-3 SINGIDA FOUNTAIN GATE

Mkurugenzi wa ufundi wa Singida FG, Ramadhan Swanzurimo ametozwa faini ya Million moja [1,000,000] kwa kosa la kuingia kwenye eneo la kiufundi la mchezo.

BODI YA LIGI ITAKUSANYA JUMLA YA KIASI CHA MILLION 11.5 KUTOKANA NA MAKOSA YALIYOTENGEKA KWENYE MICHEZO YA LIGI KUU PEKEE.

LIGI YA CHAMPIONSHIP

MECHI NAMBA 67: BIASHARA UNITED 2-1 MBEYA CITY

Kocha wa Mbeya City, Salum Mayanga ametozwa faini ya Laki tano [500,000] kwa kosa la kuwatilea lugha chafu waamuzi wa mchezo.

Kocha wa viungo wa Mbeya City, Paul Nonga ametozwa faini ya Laki tano [500,000] na kufungiwa michezo mitatu kwa kosa la kuwatolea lugha chafu waamuzi.

MECHI NAMBA 76: STAND UNITED 0-1 MBEYA KWANZA

Stand United imetozwa faini ya laki tano [500,000] na kucheza bila mashabiki michezo mitano (5) kwa kosa la mashabiki wake kuingia uwanjani kuwapiga waamuzi.

LIGI DARAJA LA KWANZA:

MECHI NAMBA 5A: AFRICAN LYON vs KILUVYA FC

Klabu ya kiluvya imepewa ushindi wa alama tatu (3) na magoli matatu (3) katika mchezo huo ambao haukufanyika kwasababu wachezaji wote wa African Lyon hawakuwa na leseni..

MECHI NAMBA 12A: LIPULI FC VS DAR CITY

Lipuli imetozwa faini ya million tatu [3,000,000] na kutozwa alama 15 kwa kosa la kushindwa kufika uwanjani.

Klabu ya Dar City imepewa alama tatu (3) na magoli matatu (3).

BODI YA LIGI KUU KUVUNA MILLION 16 JUMLA KUTOKANA NA MAKOSA YOTE

Makala Nyingine

More in NBC Championship