Connect with us

NBC Championship

MBUNI FC KUTUPA KARATA YAKE YA 11 HII LEO .

Klabu ya soka ya Mbuni Fc hii leo saa 10:00 Jioni itakuwa uwanjani kutupa karata yake ya 11 katika mwendelezo wa ligi ya Nbc championship msimu wa mwaka 2023/24 katika uwanja wa Black Rhino Karatu dhidi ya Polisi Tanzania.

Klabu ya Mbuni kiasili Uwanja wake wa nyumbani ni Sheikh Amri Abeid kaluta mkoani Arusha, Licha ya kutumia uwanja huo klabu Mbuni bado Uwanja wake wa nyumbani ni Sheikh Amri Abeid,na pia wataendelea kuutumia Uwanja huo mpaka Msimu utakapotamatika.

Leo klabu hiyo itautumia Uwanja wa Black Rhino Karatu kwasababu ya matumizi mengine ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, hivyo imewalazimu kutumia Uwanja mwingine tofauti na Sheikh Amri Abeid .

Kufuatia kuwa na idadi chache ya viwanja vinavyokidhi hadhi ya Nbc Championship ndani ya Jiji la Arusha wameamua mchezo huo uliopaswa kuchezwa siku ya Jumamosi ya tarehe 18.11 .2023 saa 10:00 ambao umerudishwa nyuma kwa siku 1 utapigwa leo saa 10:00 Jioni katika wilaya ya Karatu Mjini Karatu .

Uwanja wa Black Rhino una ubora na miundo mbinu rafiki na wezeshi na una pitch ya kisasa kabisa na huu ni uwanja namba moja kwa ubora katika matumizi ya championship.

Klabu hiyo imetangaza kiingilio cha mchezo huo wa leo,

Kiingilio ni shilingi 2,000/= .

Takwimu za Mbuni fc Msimu wa. 2023/24 katika mechi 10 .

Ushindi Mechi 5

Sare Mechi 3
Kufungwa mechi 2.

Makala Nyingine

More in NBC Championship