Connect with us

Top Story

PITSO AMTAKA MCHEZAJI WA ZAMANI KUWA KOCHA.

Mwaka 2019, nyota wa zamani wa klabu ya Superaport, Mamelodi Sundowns, Kaizer Chiefs, na Royal Eagles na timu ya Taifa ya Afrika Kusini Katlego Mphela alitangaza kistaafu kucheza soka na kuhamia biashara ya uuzaji wa magari.

Safari yake ya soka ilianzia kwenye klabu ya Jomo Cosmos na baadae akaelekea nchini Ufaransa kwenye klabu ya Strasbourg mwaka 2004 kabla ya kurejea tena Afrika Kusini mwaka 2006.

Kwa kipindi cha hivi karibuni Mphela alijiingiza katika biashara ya magari kwaajili ya kuitunza familia yake. Kocha wake wa zamani Pitso Mosimae ameonyesha kufurahishwa na namna ambavyo Mphela anaendelea kupambana.

Ninafurahi anafanya kazi nyingine nje ya mpira wa miguu. Nimesikia kuwa anafanya kazi ya uuzaji wa magari. Ni wazo zuri sana, anaweza kufanikiwa, amepata jina lakini pia bado anapenda mpira najua. Anaweza akafanya kazi ya kufundisha kama kazi ya ziada, afate kile anachokipenda.

Natumaini atatusaidia kwenye shule ya mpira ya Pitso Mosimane, wakati anafanya kazi yake ya muda na lazima aende akasomee ukocha na apate sifa za kuwa kocha, anaakili sana, anajua nini cha kufanya.

Atakuwa kocha mkubwa kama makocha wengine ambao wanafundisha kama vile Morgan Gould, Dillon Sgeppard, makocha wote waliokuwa sehemu ya mpira wa miguu. Alikuwa sehemu ya mpira wa miguu, lakini wacha afate kile anachokifanya kwasasa ili aendelee kuitunza familia yake.

Kadri muda unavyoenda, taratibu ataanza kutafuta sifa za kuwa kocha na kama atakutana na ugumu katika hilo, nitamsaidia, anajua kuwa anaweza kunipigia na tukaongea na Walter Steenbok, na akapata sifa kama hao makocha wengine, kwanini isiwezekane?.

Anaweza kuendelea na biashara yake lakini pia akautumikia mpira. Amepiga hatua kubwa sana, ameelekea kwenye uelekeo sahihi na hicho ndicho tunachokitaka kwa wachezaji wetu wa zamani.

Kila la kheri muuaji.

Pitso Mosimane akizungumzia swala la Mphela kurejea tena kwenye mpira wa miguu baada ya kustaafu.

Kama Mphela atachagua kuikubali nafasi aliyopewa na Pitso Mosimane tunaweza kumshuhudia akifuata nyayo za kocha wa sasa wa Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena ambaye amekuwa na kiwango bora sana.

Makala Nyingine

More in Top Story