19:00 GAMBIA vs IVORY COAST
UWANJA: Benjamin Mkapa
Uwanja wa Benjamin Mkapa upo “Busy” sana kipindi hiki cha michuano ya kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia 2026 zitakazo fanyika katika nchi za Mexico, Marekani na Canada.
Mataifa mawili yameuchagua uwanja huu kuutumia katika mechi zake baada ya nchi hizo kukosa viwanja vinavyokidhi vigezo vya kuchezea mashindano hayo.
Mataifa hayo ni Burundi pamoja na Gambia ambayo yapo kundi F linaloongozwa na timu ya Taifa ya Gaboni kwa sasa iliyo na alama sita (6). Burundi imeutumia uwanja huu katika michezo yake miwili dhidi ya Gambia wakati wakiibuka na ushindi wa goli 3-2, na katika mchezo wa leo dhidi ya Gabon uliomalizika kwa timu hiyo kupoteza kwa magoli 2-1.
Gambia Jumatatu ya kesho itashuka dimbani kutupa karata yake ya pili katika michuano hii kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 1:00 Jioni kuikaribisha Ivory Coast ya Sebastien Haller ambayo tayari ipo nchini kwaajili ya mchezo huo.
Ivory Coast imetoka kupata ushindi wa goli 9-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Seychelles. Kundi F lina timu sita (6) na kila timu imecheza walau mchezo mmoja hadi hivi sasa, timu hizo ni Gabon, Ivory Coast, Burundi,Gambia,Kenya na Seychelles.