Connect with us

EPL

ONANA AJIVUNJA TIMU YA TAIFA.

Golikipa wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Cameroon Andre Onana (27) hatakuwa sehemu ya kikosi cha Cameroon kitakacho ikabili timu ya Taifa ya Libya Jumanne hii, baada kuumia katika mchezo dhidi ya Mauritius waliposhinda goli 3-0 kwenye mchezo wa kundi D wa kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia.

Onana amerejea Manchester United kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu zaidi kwenye jeraha ambalo bado halijafahamika. Shirikisho la soka la Cameroon pia halijatoa taarifa kamili kuhusu majeraha ambayo mlinda lango huyo ameyapata.

Taarifa kadhaa zinaeleza kuwa Onana anaogopa kukosa mchezo wowote wa Manchester United akihofia kupoteza namba kwenye kikosi cha kwanza hivyo amejivunja ili akaungane na kikosi hicho kwaajili ya mchezo wa Ligi kuu England dhidi ya Everton Jumapili ijayo.

Ikumbukwe kuwa mlinda lango huyo aliwahi kustaafu kuitumikia timu ya Taifa ya Cameroon na baadae akatangaza kurejea na kuna uwezekano wa kutoshiriki fainali za AFCON 2023 zitakazofanyika January 2024 nchini Ivory Coast akihofia kupoteza nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Manchester United.

Makala Nyingine

More in EPL