Connect with us

Yanga

ULOZI CHANZO CHA KUTOFANYA VIZURI FISTON.

Nyota wa zamani wa klabu ya Young Africans ya Jijini Dar Es Salaam, raia wa Burundi, Fiston Abdulrazack ameweka wazi kuwa sababu ya kushindwa kwake kufanya vizuri ni pamoja na Kupigwa ‘misumari’ na wachezaji wengine.

Fiston ameeleza kuwa hakuna nyota anayependa kufeli kwenye mpira lakini mambo hubadilika kulingana na mambo unavyoyakuta kwenye timu husika.

Hayo mambo mengine ya misumari nilipokuja nilikuwa sijui lakini mimi nikashangaa kwanza swali la kwanza waandishi wananiuliza wewe umejipangaje ?, wakanitajia majina ya wachezaji wakubwa wamepita hapa lakini wamefeli, wewe umejipangaje juu ya hilo?.

Mimi nilikuwa naona hawa wananichukuliaje huwa wanaangalia TV ? au wananionaje ? Nilikuwa nashindwa kuwaelewa.

Mwisho wa siku nilikuja kuwaelewa walikuwa wanamaanisha kitu gani.

Vitu vingine ni siri huwezi tu kuviweka wazi kwenye nyombo vya habari kama hivi, lakini mambo ya ‘misumari’ ni kweli kabisa .

Unajua mimi ni yule mtu ambaye naamini sana katika Mungu, lakini nilikuja kuamini kwamba ‘Misumari pia ipo.

Hakuna Binadamu anayependa kufeli, sio kwamba naweza kufurahia kitendo cha mimi kushindwa na kutokufanya vizuri.

Kama nikirejea leo nitakuwa nimejiandaa sawasawa kama mwanajeshi anayeenda vitani vile, nihakikishe kwamba misumari hainipati, nitakuwa nipo imara kabisa.

Fiston Abdulrazack akieleza chanzo cha kutokufanya vizuri akiwa na Young Africans.

Misumari ni uchawi unaofanywa na wachezaji wanaocheza kwenye namba moja ili mmoja aumie na mwingine apate nafasi ya kucheza au mmoja afanye vibaya na mwingine apate nafasi ya kucheza. Wachezaji wengi hushindana katika haya mambo ili wapate nafasi ya kucheza kuliko uwezo na kujituma mazoezini ili kocha amuamini.

Fiston alisajiliwa na kikosi cha Yanga kikiwa na matarajio makubwa juu yake lakini mambo hayakwenda vizuri kwa nyota huyo raia wa Burundi.

Mshambuliaji huyo yupo nchini Tanzania na timu ya Taifa ya Burundi inayotumia uwanja wa Benjamin Mkapa kama uwanja wake wa nyumbani kwenye michezo ya kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia 2022.

Makala Nyingine

More in Yanga