Connect with us

Top Story

KARUME BOYS WAKUTANA NA RAIS MWINYI IKULU.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Wachezaji wa Karume Boys katika hafla ya chakula cha mchana iliyofanika leo Ikulu Zanzibar na kuwapongeza kwa kuchukua kombe la CECAFA chini ya umri wa miaka 15.

Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe Tabia Mwita amesema kuwa tayari wameshawafungulia wachezaji wote wa Karume Boys akaunti za benki kwa ajili ya kuhifadhi fedha zao watakazoingizwa kama pongezi ya kutwaa ubingwa wa CECAFA U15 Boys Championship 2023.

Mhe.Tabia ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya chakula cha pamoja Ikulu visiwani Zanzibar kwa mualiko wa Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi ambapo amesema hadi sasa fedha za ahadi kutoka kwa viongozi, taasisi na watu mbalimbali zinafikia shilingi milioni 95 za kitanzania.

Mhe Tabia amesema baada ya kukusanya fedha zote hizo watakaa chini na wazazi wa wachezaji hao ili kuhakikisha kila mchezaji anapata anachostahili kwenye akaunti yake na kuwasaidia kwenye matumizi sahihi ya fedha hizo.

Makamu wa Rais wa Yanga SC, Arafat Haji amekabishi kitita cha shilingi milioni 2.5 kwa KARUME BOYS mabingwa wa CECAFA U15 mwaka 2023, mashindano yaliyofanyika nchini Uganda.

Arafat Haji ambae pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Zanzibar ZIC amemkabidhi kiasi hicho cha shilingi milioni 2.5 za ahadi yake ya magoli ya Karume Boys kwa Mhe Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita.

Makala Nyingine

More in Top Story