Christopher Nkunku na Romeo Lavia kila mmoja anakaribia kucheza kwa mara ya kwanza Chelsea baada ya kufanya mazoezi kujiandaa na mtanange utakao wakutanisha na Newcastle kwenye mechi ya Ligi Kuu nchini Uingereza (EPL).
Huku wachezaji wenza wa Chelsea wakishiriki katika michezo ya kimataifa kwingineko, Nkunku na Lavia walipigwa picha wakifanya mazoezi pamoja huko Cobham Jumatatu jioni. Kufuatia ripoti za awali kwamba wote wanakaribia kuwa fiti kabisa na mechi zao za kwanza, inaongeza uwezekano kwamba wote wanaweza kucheza dhidi ya Newcastle.
Wote wawili walisajiliwa majira ya kiangazi, Nkunku aliyegharimu pauni milioni 53 ($67m), na pauni milioni 58 ($74m) Lavia bado hawajaichezea Chelsea. Mchezaji huyo wa zamani, ambaye aliifungia RB Leipzig mabao 58 katika kampeni mbili pekee za awali, alikuwa amefanya vyema katika mechi za kujiandaa na msimu kabla ya kupata jeraha la goti katika mechi ya kirafiki dhidi ya Borussia Dortmund. The Blues baadaye waliwashinda Liverpool kwenye saini ya Lavia lakini tatizo la kifundo cha mguu limemfanya akose kucheza.
Nilifanya mazungumzo na Christopher na akaniambia alitaka kuhusika katika mchezo unaofuata dhidi ya Newcastle United baada ya mapumziko ya kimataifa. Nadhani yuko karibu na anaendelea vizuri sana. Tunafurahi sana naye kwa jinsi anavyopata ahueni. Yeye ni mtaalamu sana. Romeo Lavia pia nae yuko karibu kurudi uwanjani.
Mauricio Pochettino alisema kabla ya kumenyana na Manchester City hivi karibuni.
Baada ya kuanza vibaya msimu huu, Chelsea hatimaye wanaonekana kurudi taratibu kwenye ubora na wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya nane zilizopita katika mashindano yote, wakishinda tano kati ya hizo. Wakiwa wameilazimsha sare Manchester City kwa kufungana 4-4 katika mechi ya Ligi Kuu nchini Uingereza (EPL) kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa. Chelsea wanahitaji kuendeleza kasi hiyo katika mechi zijazo dhidi ya Newcastle, Brighton, Manchester United, Everton na Sheffield United katika muda wa wiki nne zijazo.