Nyota wa klabu ya Karlslunds Idrottsförening FK inayoshiriki Ligi daraja la pili nchini Sweden na timu ya Taifa ya Tanzania Kwesi Kawawa amefunguka na kusema licha ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Morocco hapo jana bado kuna nafasi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia.
Najisikia vizuri kulitumikia Taifa langu kwa mara ya kwanza, nina furaha kwaajili ya nchi yangu, tutaendelea kupambana lakini mara hii hatujapata ushindi.
Bado tunanafasi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia kwa asilimia mia, makosa niliyofanya hayana sio tatizo nitayafanyia kazi, kwa wakati mwingine nitafanya vizuri zaidi.
Nina furaha sana na siwezi kuelezea, nina wiki mbili tangu niko hapa, nina furaha sana, watu wake ni wakarimu na ni wazuri, nitarejea tena na nitalifanya Taifa lijivunie.
Kwesi Kawawa, Golikipa wa timu ya Taifa ya Tanzania.
Kwesi Kawawa alikuwa na kiwango bora sana jana licha ya kuwa huu ni mchezo wake wa kwanza akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania, mchezo ambao ameruhusu magoli mawili.
Taifa Stars ilikubwali kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa timu ya Taifa ya Morocco, mchezo ambao ulichezwa Jumanne, November 21 katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar Es Salaam. Huu ulikuwa mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia baada ya ule wa awali dhidi ya Niger kuibuka na ushindi wa goli 1-0 ugenini.
Kawawa anatajwa kuwa miongoni mwa nyota ambao wataunda kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kitakachoshiriki fainali za mataifa ya Afrika [AFCON] zinazotazamiwa kuchezwa mwezi January chini Ivory Coast.