Connect with us

NBC Premier League

ARAFAT: SKANDA KAONYESHE KILE HERSI AMESHINDWA.

Klabu ya Ihefu kutoka Mbarali mkoani Mbeya inayoshiriki Ligi kuu kandanda Tanzania Bara imemtambulisha rasmi Biko Armando Scanda kuwa afisa mtendaji mkuu [CEO] wa klabu hiyo. Biko kabla ya kuteuliwa kuwa CEO alikuwa mchambuzi wa maswala ya soka hasa akibobea zaidi katika uchumi wa klabu lakini pia meneja wa maudhui wa kampuni ya Ulinzi ya K4S hapa nchini.

Baada ya utambulisho huo mpya uliofanywa na klabu ya Ihefu, wadau na wapenzi wa soka nchini kila mmoja kwa namna yake ameupongeza uongozi wa klabu ya ihefu kwa namna ulivyofanya maamuzi ya kumteua Biko kuwa Mtendaji wake mkuu.

Hapa Ihefu wamepata mtu wa maana.

Shabiki mmoja aliandika.

Hongera sana kaka lakini jua una mtihani mkubwa kama wa Neville.

Shabiki meingine pia aliandika.

Hongera sana mkuu, njia nzuri ya vijana kuaminiwa inazidi kuhalalishwa na watu kama nyie. Ila sasa jua watu watakuangalia na kukupima kwa kipimo ulichokuwa ukiwapimia wengine kipindi upo nje ya gurudumu la uongozi wa mpira, kazi ni kwako.

Shabiki mwingine alizungumza.

Makamu wa Rais wa klabu ya Young Africans Arafat Haji naye ni miongoni mwa wale waliotoa pongezi za dhati kwa Biko akimtaka akakionyeshe kile alichokuwa ana kizungumza kwenye vyombo vya habari na kile alichoshindwa kukionyesha Rais wa klabu ya Yanga Eng. Hersi Ally Said.

Kila la Kheri dogo, sasa ile Football Economy ambayo Eng. Hersi haijui tukaione Ihefu, tuone jezi nzuri, tuone wachezaji World Class na wadhamini pamoja na event zilizo kamilifu sana.

Arafat Haji, Makamu wa Rais wa klabu ya Young Africans.

Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Simba Imani Kajula naye alikuwa sehemu ya wale waliotoa pongezi kwa Biko Scanda baada ya kutambulishwa rasmi kuitumikia klabu hiyo ya Ihefu.

Hongera sana Biko, najua kwa dhati uwezo wako na kubwa zaidi shauku yako ya kuleta mabadiliko. Kila la kheri na Mungu akuongoze.

Imani Kajula, Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Simba.

Biko Scanda ana kibarua kizito kwasasa kwenye klabu hiyo cha kuhakikisha inabaki Ligi kuu kandanda Tanzania Bara na inafanya vizuri katika mashindano mengine itakayoshiriki.

Kila lakheri katika utumishi wako nyota Biko Armando Scanda.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League