Connect with us

NBC Premier League

FIFA YAIFUNGIA SIMBA KUFANYA USAJILI.

Klabu ya soka ya Simba imefungiwa kufanya usajili wa wachezaji na shirikisho la soka Duniani [FIFA] hadi pale itakapoilipa klabu ya Teungueth ya Senegal sehemu ya pesa ilizozipata Simba baada ya kumuuza kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Pape Ousmane Sakho.

Kwa mujibu wa mkataba walioingia klabu ya Simba na Teungueth wakati wa kuuziana nyota huyo ni kuwa mahali popote klabu ya Simba itakapomuuza nyota huyo, klabu ya Teungueth itanufaika na mauzo hayo.

Klabu ya Simba ilikiuka makubaliano hayo na haikuilipa klabu ya Teungueth jambo ambalo lilipelekea klabu hiyo kuipeleka FIFA klabu ya Simba ikidai malipo baada kumuuza kwenda klabu ya Quevilly Rouen Metropole ya Ufaransa.

Simba ilitakiwa kutekeleza malipo hayo ndani ya siku 45 tangu maamuzi ya shirikisho la soka FIFA yalipotolewa lakini ilishindwa kufanya hivyo.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League