Connect with us

NBC Premier League

NAMUNGO YAINYANYASA IHEFU

Namungo imepata ushindi wake wa kwanza Nyumbani msimu huu wakiifunga Ihefu kwa mabao 2-0 na kupata alama 3 muhimu zilizowasogeza mpaka nafasi ya 9 wakifikisha alama 11.

Ihefu waliuanza mchezo vibaya baada ya kujikuta wako pungufu dakika ya 10 tu ya mchezo baada ya Kenneth Kunambi kuunawa mpira akiuzuia kuingia langoni na kuonyeshwa kadi nyekundu, Ihefu kulazimika kucheza dakika takribani 80 za mchezo mzima wakiwa 10 kiwanjani. Hata hivyo Penati ikiyotokana na tukio hilo, ilipanguliwa vema na golikipa Fikirini Bakari.

Namungo walishindwa kuitumia vizuri faida ya uchache wa wachezaji wa Ihefu dakika 45 za kwanza za mchezo wakishindwa kummsumbua vilivyo Fikirini Bakari na safu yake ya Ulinzi licha ya kufika mara nyingi golini kwa wapinzani. Utasifu nidhamu kubwa ya mchezo waliyoiweka Ihefu.

Dakika ya 35 ya mchezo, Ihefu walishindwa kuihimili mashinikizo ya Namungo kwa muda mrefu, krosi murua kutoka kwa Nahodha Jacob Massawe iliunganishwa vizuri na Pius Buswita kuipa timu yake bao la kuongoza akiwaacha Walinzi na kipa wao wasiwe na la kufanya.

Kipindi cha pili kilianza na mabadiliko kwa ihefu, John Kitenga anachukua nafasi ya Mubarak Amza kipindi hiki cha pili yakiwa ni mabadiliko ya kiufundi kwenda kuipa nguvu safu ya ulinzi pamoja na Rashid Juma kumpisha Shaaban Msala kwenye eneo la Kiungo cha Ulinzi kupunguza kasi ya mashambulizi ya Namungo.

Ihefu walionekana kuutuliza mchezo baada ya mabadiliko hayo na kuwafanya Namungo wacheze zaidi kwenye nusu yao. Ni kama waliwaruhusu wachezee mpira lakini kwenye eneo lao na wao kufunga milango yao ya ulinzi. Mwalimu Basena akaona dakika 20 za mwisho aingize kasi mpya ya ushambulizi kujaribu kusawazisha goli kwa kumuingiza Nassor Saadun akichukua nafasi ya Joseph Mahundi, akiingia pia Jaffary Kibaya nafasi ya Ismail Mgunda na Never Tigere nafasi ya Rajab Athuman, dakika ya 70.

Dakika ya 78, Hamadi Majimengi aliendelea kuhakikisha kuwa Namungo wanaondoka na alama zote 3 baada ya kukwamisha kimiani bao la pili akimalizia mpira uliopanguliwa na Fikirini Bakari wakati akiokoa shuti kali la Frank Domayo. Namungo 2-0 Ihefu. Muda huo huo anammpisha Hashim Manyanya.

Seidou Blandja anachukua nafasi ya Reliants Lusajo dakika ya 88

Namungo waliendelea kuutawala Mchezo baada ya hapo mpaka dakika ya 90 kwa filimbi ya Muamuzi Liston Hiyari na mchezo kumalizika kwa Namungo kuibuka na ushindi wa 2-0.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League