Connect with us

FIFA World Cup

DIARRA AIPELEKA MALI NUSU FAINALI WORLD CUP.

Fainali za kombe la Dunia chini ya miaka 17 zinazofanyika nchini Indonesia zimefika hatua ya nusu fainali baada ya hii leo kutamatika michezo miwili ya hatua ya robo fainali.

Timu nane ziliingia katika hatua ya robo fainali ambapo kutoka Bara la Afrika ziliingia timu mbili (2) ambazo ni Mali na Morocco, Ulaya ikawakilishwa na timu tatu (3), America Kusini ikawakilishwa na timu mbili (2) Brazil na Argentina, huku Asia ikiwakilishwa na timu moja (1) Uzbekistan

Mchezo wa mapema uliikutanisha timu ya Taifa ya Ufaransa dhidi ya Uzbekistan mchezo ulioshuhudia Ufaransa ikisonga hatua ya nusu fainali baada ya kuichapa Uzbekistan goli 1-0, goli lililofungwa na Bouneb dakika 83 ya mchezo.

Mchezo wa pili ulizikutanisha timu kutoka Afrika timu ya Taifa ya Mali dhidi ya Morocco, mchezo ulioipa nafasi Mali kusonga mbele baada ya ushindi wa goli 1-0, goli lililofungwa na Diarra dakika ya 81.

Jana timu ya Taifa ya Brazili iliondoshwa na Argentina baada ya kipigo cha magoli 3-0 na Ujerumani ilisonga mbele baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Hispania.

Hivyo hatua ya nusu fainali itachezwa na timu za Mali, Ujerumani, Argentina na Ufaransa.

Baada ya matokeo hayo Argentina itakutana na Ujerumani November 28 saa 11:30 Asubuhi, huku nusu fainali ya pili ikipigwa siku hiyo hiyo majira ya saa 15:00 kati ya Mali na Ufaransa.

Mchezo wa fainali ya michuano hii utapigwa December 2, majira ya saa 15:00 huko nchini Indonesia.

Makala Nyingine

More in FIFA World Cup