Connect with us

Manchester City

GUARDIOLA: MTAMUONA DE BRUYNE SIKUKUU.

Pep Guardiola ametoa taarifa kuhusu tarehe ya kurejea kwa Kevin De Bruyne huku nyota huyo wa Ubelgiji akiendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji wa nyama za paja.

De Bruyne amesalia nje ya uwanja tangu katikati ya Agosti baada ya kulazimishwa kutoka nje dakika ya 23 katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya klabu hiyo dhidi ya Burnley. Sasa kocha wa City Guardiola ametoa taarifa ya matumaini kuhusu tarehe ya kurejea kwa Mbelgiji huyo huku akidokeza kwamba mashabiki wa City wanapaswa kufurahia kipindi hiki cha sikukuu.

Ningependa kuwa naye (De Bruyne) msimu wote lakini amefanyiwa upasuaji na lazima apone vyema. Mwisho wa Desemba au [katika] mwaka mpya utakuwa Mwaka Mpya wa Furaha kwa kila mtu!

Tuna mazoezi sasa lakini tutaona alasiri hii… sina matumaini kuhusu habari njema kwa baadhi ya watu kurudi… John Stones anazidi kuwa bora… Sio kucheza lakini labda dakika chache kwa mechi moja ijayo.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mechi ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya RB Leipzig.

Akiwa tayari amefuzu kwa hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kukusanya pointi 12 kutokana na mechi nne, Guardiola anatarajiwa kutambulisha sura mpya huku klabu hiyo ya Manchester City itakapomenyana na RB Leipzig Jumanne.

Makala Nyingine

More in Manchester City