Manchester United imekuwa klabu ya kwanza kuweka rekodi ya hati safi (clean sheet) 500 kwenye Ligi Kuu ya nchini Uingereza (EPL) baada ya ushindi wa 3-0 Jumapili dhidi ya Everton katika uwanja wa Goodson Park.
Alejandro Garnacho alikuwa ndiye aliyetengeneza vichwa vya habari, kutokana na jitihada zake za kusisimua baada ya goli lake la kuvutia alilofunga kwa mtindo wa tiktaka, huku mabao ya Marcus Rashford na Anthony Martial yakiihakikishia ushindi muhimu kwenye Uwanja wa Goodison Park. Lakin Manchester United walilazimika kusimama kidete katika hatua fulani za pambano hilo, haswa katika kipindi cha kwanza ambapo Everton walikuwa wakitafuta sana bao la kusawazisha.
Kobbie Mainoo aliondoa juhudi za Dwight McNeil nje ya mstari, huku Andre Onana akipangua shuti bora kutoka kwa Idrissa Gueye baada tu ya Rashford kufanya matokeo kuwa 2-0. Lilikuwa ni la tatu mfululizo la kupanguliwa kwa Mcameroon huyo na mabeki wake, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Fulham na Luton Town.
Onana kwa sasa anashika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya Ligi ya Premia ya Golden Glove kwenye mechi yake ya tano bila kufungwa msimu huu , huku Chelsea wakiwa na jumla ya hati safi 476, ikifuatiwa na Liverpool wenye 460 na Arsenal wakiwa na hati safi 456 pekee.
Wingi wa hati safi za United unashikiliwa na magoli kipa watatu, huku David De Gea akiongoza akiwa na hati safi 147. Peter Schmeichel anafuatia, akiwa na 112, huku van der Sar akiwazuia washambuliaji wa upinzani mara 94 kwa United. Fabien Barthez 34, Roy Carroll 26, Tim Howard, Tomasz Kuszczak wote wakiwa na hati safi 16, Raimond van der Gouw (12), Mark Bosnich (11) na Anders Lindegaard (9) pia ni wachangiaji wakuu kwenye rekodi hiyo. Kwa wachezaji waliokamilika huko, huku magolikipa wafuatao United pia wakichangia widadi ya hati safi katika Ligi Kuu nchini Uingereza (EPL): Ben Foster, Sergio Romero, Gary Walsh, Dean Henderson, Kevin Pilkington, Victor Valdes, Paul Rachubka, Ben Amos na Joel Pereira.