Connect with us

Makala Nyingine

NGAO YA JAMII – LIGI KUU WANAWAKE INAKUJA.

Timu nne za Wanawake zitashiriki michuano ya ngao ya jamii na baadhi ya wachezaji wamefunguka mikakati yao kwenye kipute hicho kinachoanza Disemba 9 hadi 12, Uwanja wa Azam Complex.

Yanga wanaanza na Simba huku Fountain ikipangwa na bingwa wa Ligi Kuu, JKT Queens. Kiungo mshambuliaji wa Simba Queens, Vivian Corazone alisema wamefurahi kupangwa na Yanga na utakuwa mwanzo mzuri kwao kujua wanaianza vipi Ligi Kuu.

Ni mashindano tunayocheza kwa mara ya kwanza, najua kila timu imejipanga vizuri kwa mashindano na sisi tunaendelea kujifua kuweka historia nyingine.

Alisema kiungo wa Simba Queens Vivian Corazone.

Kiungo mkabaji wa JKT Queens, Donisia Minja alisema kama wachezaji wamepokea vizuri kuanza na Fountain Gate Princess lakini maandalizi yao mazuri ndio yatawavusha kwenda fainali.

Kwa upande wa beki wa Yanga, Lucy Pajero alisema,

Nataka kufanya makubwa kwenye mashindano hayo na kubeba ubingwa.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine