Connect with us

CAF Champions League

AL HILAL YAWAITA MASHABIKI KWA MKAPA.

Klabu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan imewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo wao unaofuata wa Ligi ya mabingwa Barani Afrika dhidi ya ES Tunis ya Tunisia, mchezo utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar Es Salaam.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram klabu hiyo imeandika maneno ya kiswahili ikiwaomba wapenda soka kwa umoja wao kujitokeza kwenye michezo yake yote ya nyumbani kuanzia ule wa ES Tunis.

Kutoka nchi ya amani na upendo Tanzania tunatarajia kuonekana tofauti katika toleo la sasa la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wazao wa Hayati kiongozi Julius Nyerere, tunasubiri msaada wenu katika ziara zenu za ardhi yetu.

Ardhi yetu ni ardhi yako.

Waliandika Al Hilal kwenye ukurasa wao wa Instagram.

Al Hilal ilichagua kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa katika michezo yake yote ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya nchi ya Sudan kuwa kwenye machafuko hali iliyopelekea pia Ligi ya nchi hiyo kusimama.

Makala Nyingine

More in CAF Champions League