Connect with us

Simba

BENCHIKHA AKUTANA NA WACHEZAJI SIMBA SC.

Utambulisho wa wachezaji kwa benchi jipya la ufundi umefanyika huko katika kikosi cha Wekundu wa Msimbazi Simba, lengo likiwa ni kufahamiana na kocha kuelezea mpango kazi wake kama kocha mkuu.

Abdelhak Benchikha amefanya kikao na wachezaji wa Simba kwa mara ya kwanza tangu atambulishwe rasmi jana.Kikao na wachezaji hao ambao wanajiandaa na mechi ya pili ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Jwaneng Galaxy mechi inayopigwa nchini Botswana.

Ikumbukwe katika mchezo wa kwanza wa Simba SC ililazimishwa sare ya 1-1 na timu ya Asec Mimosas kutoka nchini Ivory Coast, katika mchezo uliopigwa Jumamosi iliopita katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam.

Makala Nyingine

More in Simba