Connect with us

Betting Tips

MKEKA WAKO

Galatasary na Manchester United wanakutana leo huko Uturuki huku kumbukizi zikionyesha United alinyukwa kwenye mchezo wa kwanza tena Old Trafford huku mzimu wa Wilfried Zaha ukiendelea kuwasonga. Ni vita kubwa leo ya alama 3 ili kutafuta nafasi ya kufuzu raundi ya 16 huku Bayern akiwa tayari ashajihakikishia pengine kushindilia leo dhidi ya Copenhagen.

Timu zote mbili hizi zimetoka kufaidi utamu wa ushindi wa magoli zaidi ya 2.5 bila BTTS lakini tunatarajia Goals Galore kwenye mchezo huu wa leo. Kila mtu anataka ushindi mchezo huu na ushindi magoli. Tofauti ya alama 1 tu kati yao huku kila timu ikiskilizia na matokeo ya Bayern.

DONDOO : MAGOLI ZAIDI YA 2.5/TIMU ZOTE KUFUNGANA

Wakati wowote ule haijalishi nafasi ya timu hizi mbili wanapokutana kinapigwa haswa. Lakini Real Madrid wamekuwa na kiwango bora kuliko Napoli hivi karibuni licha ya timu zote kupata matokeo kwenye ligi zao za nyumbani. Madrid akimmfunga Cadiz 3-0 na Napoli akimchapa Atalanta 2-1.

Madrid wanaongoza kundi wakiwa na alama 12 huku Napoli wakiwa na alama 7 na wanatambua umuhimu wa kupata alama 3 leo huku Madrid naye atataka kuhakikisha kabisa kuwa anasonga raundi ya 16 mapema. Mechi 4 kati ya 5 za Madrid zimeisha kwa magoli zaidi ya 2.5. Madrid kushinda leo pia ni asilimia kubwa hasa akiwa nyumbani Bernabaeu.

DONDOO : REAL MADRID USHINDI

Wote wameshinda michezo 3 kati ya 5 za mwisho. Lakini kwenye kundi hili C michezo ya mwisho iliisha kwa Arsenal kuichapa Sevilla 2-0 huku Lens wakiangukia pua kwa kupigwa 1-0 na PSV.

Arsenal anaongoza kundi akiwa na alama 9 lakini kati yake na Lens ni alama 4. Arsenal wanachua alama 12 ni muhimu kujihakikishia kufuzu hivyo wataitolea macho hii mechi leo. Lakini Lens pia wanajua alama 8 zitwasogeza kwenye malengo yao.

DONDOO : ARSENAL USHINDI

Ipswich wapo nafasi ya 2 kwenye msimamo wa Championship lakini mechi yao ya mwisho waliambulia kipigo cha 2-0 mbele ya WBA lakini na Millwall naye aliye nafasi ya 18 alitandikwa vilivyo nyumbani kwake 3-0 na Coventry.

Ipswich watataka kurudi kwenye mbio zao za kupanda daraja na bila shaka hawatoruhusu Millwall wasimame kwenye njia yao.

DONDOO : IPSWICH USHINDI

Mechi ngumu sana hii huko Ligue 1 leo. Timu hizi mbili zimekuwa na panda shuka msimu huu lakino kipigo cha 3-1 kutoka kwa Stade Brestois kimekuja kama mshituko kwa Montpellier. Wakati huo Clermont Foot wakipigwa 3-0 dhidi ya Lens.

Pamoja na yote tunaipa nafasi kubwa montpellier kupata matokeo leo mbele ya Clermont Foot.

DONDOO : MONTPELLIER USHINDI

Makala Nyingine

More in Betting Tips