Connect with us

NBC Premier League

COASTAL UNION YAITANDIKA GEITA GOLD

Coastal Union wameibuka kutoka kwenye kufungwa 2-1 na Singida Big Stars na kupata ushindi wa 3-1 hii Leo dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa kwenye dimba la Mkwakwani jijini Tanga.

Geita Gold walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya ya mchezo kupitia kwa Valentino Mashaka aliyepiga shuti kali lililowababatiza mabeki na Coastal Union na mpira kummpoteza maboya golikipa Ley Ngumbi.

Wakati ikionekana kama Geita Gold wanaelekea kwenye kupata ushindi wao wa tatu mfululizo, Roland Beakou alikuwa na mawazo mengine akiisawazishia Coastal Union dakika ya 30 ya mchezo na kuipeleka timu yake mapumziko wakiwa suluhu 1-1.

Kipindi cha pili kilirejea kwa Coastal Union kuuchukua sana mchezo na dakika ya 53 tu ya mchezo Maabad Maabad alimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Greyson Gwalala kuiandikia timu yake bao la 2.

Ni kama Geita Gold walikuwa wamewaibia kitu Coastal Union kwani mashambulizi yalikuwa hayakauki golini kwao na dakika ya 59 Semfuko aliipatia Coastal Union bao la 3 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Miraji Hassan.

Coastal walifanya wanavyotaka dakika zote za mchezo mpaka kipyenga cha mwisho cha Raphael Ikambi na pengine wangeweza kufunga mabao zaidi lakini mpira ukamalizika 3-1.

Kwa matokeo hayo Coastal Union wanabadilishana nafasi na Geita Gold wakisogea kutoka nafasi ya 12 mpaka ya 9 kwa kufikisha alama 13.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League