Connect with us

Makala Nyingine

ENG.HERSI ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA VILABU AFRIKA

Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika(CAF), leo Alhamisi ya tarehe 30 Novemba,2023 imezindua rasmi Muungano wa Vilabu vya Soka Afrika(ACA-African Clubs Association) kwenye mkutano  uliofanyika  kwenye ukumbi wa Marriot Mena House jijini Cairo, Egypt ukiongozwa na Raisi ya Shirikisho hilo, Patrice Motsepe.

Viongozi kadha wa kadha wa vilabu mbalimbali vikubwa na vilivyofanya vizuri kwenye miaka ya hivi karibuni na nyakati tofauti ikiwemo kuwa na ushawishi mkubwa barani Afrika walihudhuhuria  mkutano huo uliokuwa na mlengo mkubwa wa kuinua soka la vilabu na kulifanya kuwa lenye ushindani duniani.

Azma ya umoja huu ulitambulishwa rasmi na Rais Motsepe tarehe 5 Oktoba, 2023 na pamoja na mambo mengine maagano kadhaa yalifikiwa na ndio haswa yaliyojadiliwa kwenye mkutano wa leo.

  • Kulinda na kukuza mvuto wa soka la Vilabu la Afrika.
  • Kulikuza soka la vilabu vya Afrika Kiuchumi
  • Kuhakikisha maslahi ya waamuzi yanakuwa vizuri ikiwemo kuheshimiwa, kupewa thamani, kujitegemea na kuwa wa daraja la dunia.
  • Kutengeneza ubia na ushirikiano mzuri na washika dau, wadhamini, sekta binafsi na serikali katika kujenga viwanja vyenye hadhi na viwango vya CAF na FIFA.
  • Kukuza soka la vijana na vipaji ikiwemo kukuza soka za shule kwa jinsi zote za kike na kiume.

Yote haya kwa ujumla ni kuangalia kwa namna soka la vilabu la Afrika linakuwa len ye ushindani mkubwa ili pia liweze kuwa kwenye ubora wa kidunia hata pale vilabu vya Afrika vinavyoenda kushiriki michuano ya kidunia.

Taarifa za awali zinasema kuwa kutafanyika upigaji kura wa siri kwa ajili ya kupata makao makuu ya Muungano huu wa ACA pamoja na kupata Rais wa Muungano huu. Ni viongozi wa vilabu SITA (6) tu waliopewa fursa hiyo, klabu MOJA(1)bora  kutoka kila ukanda wa kisoka.

Vilabu hivyo ni AL AHLY(UNAF), MAMELODI SUNDOWNS(COSAFA), SIMBA SC(CECAFA), TP MAZEMBE(UNIFFAC), HOROYA(WAFU A), ASEC MIMOSA (WAFU B).

Aidha, Rais wa Klabu ya Yanga Eng. Hersi Saidi amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa Muungano huo wa vilabu.

Makala Nyingine

More in Makala Nyingine