Connect with us

Serengeti Lite Women Premier League

SIMBA QUEENS TAYARI KUIKABILI YANGA PRINCESS.

Klabu ya Simba Queens imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ilala Queens ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu kandanda Tanzania Bara kwa wanawake unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Simba Queens imeichapa kipigo kizito Ilala Queens ya Ilala cha magoli 6-1 katika mchezo uliopigwa jioni ya Leo.

Magoli sita [6] ya Simba Queens yalifungwa na Asha Rashid aliyefunga magoli mawili [2], Shelder Boniface alifunga mawili [2], Zainab Mohamed akifunga goli moja [1] na goli jingine vijana wa Ilala Queens wakajifunga kupitia kwa Thabitina Salum.

Goli la kufutia machozi kwa upande wa Ilala Queens lilifungwa na Rahma Sidedi. Mchezo huo ulipigwa katika uwanja wa Bunju, Jijini Dar Es Salaam.

Huu ni mchezo wa kwanza wa kirafiki wa klabu ya Simba tangu Ligi ya wanawake itamatike msimu uliopita. Ligi hiyo pia inataraji wa kuanza hivi karibuni.

Simba Queens itacheza mchezo wa ngao ya hisani dhidi ya klabu ya Yanga Princess, December 09, 2023 saa 12:00 Jioni katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar Es Salaam.

Makala Nyingine

More in Serengeti Lite Women Premier League