Connect with us

CAF Champions League

BACCA DAY INOGESHWE NA USHINDI LEO.

Ligi ya mabingwa Barani Afrika msimu huu imekuwa na matokeo ya kushangaza sana, kila timu inafanya maajabu kwa wakati wake.

Usiyemdhania anafanya makubwa mbele ya uliyemtegemea kufanya vizuri, hii ndio Ligi ya mabingwa mpya, Ligi inayoshirikisha timu zilizo chini ya Eng. Hersi Said.

Jwaneng Galaxy iliweza kuondoka na alama tatu [3] Casablanca mbele ya Wydad AC, Medeama imepata ushindi nyumbani mbele ya CR Belouizdad hii inatisha sana.

Eng. Hersi kwa mara ya kwanza ataishuhudia timu yake leo akiwa Mwenyekiti wa klabu zote Afrika ikicheza mbele ya Mabingwa Mara nyingi klabu ya Al Ahly kutoka Misri katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar Es Salaam.

Kwa namna matokeo yanavyopatikana ni wazi leo Yanga inaweza kuibuka na ushindi na kama wakipoteza leo basi watakuwa na wakati mgumu zaidi kwenye kundi lao ambalo kila timu ina alama tatu [3] isipokuwa Yanga pekee.

Simba itakuwa kibaruani nchini Botswana, mchezo wa kwanza wa Abdelhack Benchkah, hadi hivi sasa timu hiyo ina alama moja pekee, inapaswa kushinda ili iweke mazingira mazuri kwenye kundi lake.

MICHEZO YA LEO CAF CL

KUNDI A

16:00 TP Mazembe vs Mamelodi Sundowns
20:00 FC Nouadhibou vs Pyramids FC

KUNDI B

15:00 Jwaneng Galaxy vs Simba.
23:00 Asec Mimosas vs Wydad AC.

KUNDI C

22:00 Etoile du Sahel vs Petro Atletico.

KUNDI D

17:00 Yanga vs Al Ahly

Makala Nyingine

More in CAF Champions League