Connect with us

FIFA World Cup

FAINALI KOMBE LA DUNIA U17 LEO.

Kombe la Dunia kwa vijana chini ya miaka 17 linafikia tamati hii leo kwa mchezo mmoja wa fainali kuchezwa hii leo kati ya timu ya Taifa ya Ujerumani dhidi ya timu ya Taifa ya Ufaransa.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa leo majira ya saa tisa alasiri [15:00] katika uwanja wa Manahan nchini Indonesia, ukisimamiwa na mwamuzi Espen Andreas Eskas kutoka nchini Norway.

Timu ya Taifa ya Ujerumani inapigwa chapuo ya kubeba kombe hili licha ya upinzani mkali unaotafajiwa kutolewa na timu ya Taifa ya Ufaransa hii leo.

Ufaransa imefika hatua hii baada ya kuiondosha timu ya Taifa ya Mali kwa jumla ya magoli 2-1 katika mchezo wa nusu fainali huku Ujerumani ikiifunga timu ya Taifa ya Argentina kwa changamoto ya mikwaju ya penalty 4-2 baada ya sare ya 3-3.

Ufaransa na Ujerumani zimekutana katika mchezo wa fainali wa Euro uliopigwa June 2 mwaka huu wakati ambao Ujerumani iliibuka bingwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalty 5-4 baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu [0-0].

TAKWIMU ZA TIMU ZOTE KUELEKEA MCHEZO HUO.

  • Ujerumani imecheza michezo sita [6] ya kombe la Dunia, imeshinda michezo mitano [5] na imetoa sare mchezo mmoja [1].
  • Ujerumani imefunga magoli 16 kwenye mashindano haya, kila mchezo imefunga magoli matatu [3] isipokuwa mmoja pekee dhidi ya Hispani ilifunga goli 1, imeruhusu magoli saba [7].
  • Ujerumani U17 imecheza michezo 15 katika mashindano yote mwaka huu, imeshinda michezo 11, imetoa sare michezo minne [4].
  • Ufaransa U17 imecheza michezo sita [6], imeshinda michezo mitano [5] na imetoa sare mchezo mmoja [1].
  • Ufaransa U17 kwenye mashindano haya imefunga magoli kumi [10] na imeruhusu goli moja [1] pekee.
  • Ufaransa U17 imecheza michezo kumi na tano [15], imeshinda michezo tisa [9], imetoa sare michezo mitano [5] na imepoteza mchezo mmoja [1].
  • Mwaka huu Ufaransa U17 na Ujerumani U17 zimekutana mara mbili na mara zote Ujerumani imeibuka kidedea.

Jana ulipigwa mchezo wa mshindi wa tatu kati ya timu ya Taifa ya Mali U17 dhidi ya timu ya Taifa ya Argentina na Mali ikaibuka na ushindi wa 3-0 na kuwa mshindi wa tatu [3] wa michuano hiyo.

U17 WORLD CUP 2023 FINAL.

15:00 Ujerumani vs Ufaransa.
Uwanja: Manahan Stadium, Indonesia.

Makala Nyingine

More in FIFA World Cup