Connect with us

CAF Champions League

MKAZUZU: TABULELE HAIJAFANIKIWA.

Wazo lilikuwa zuri kumleta Tabulele na kuwa sehemu ya hamasa kuelekea mchezo huo, hii ilikuwa ni kuwaita mashabiki waende uwanjani kuipa sapoti timu yao kwenye mchezo mgumu dhidi ya Ahly.

Nasema hajawafanikiwa kwasababu lengo lilikuwa mashabiki kusogea uwanjani kwa wingi zaidi lakini haikuwa hivyo, mashabiki hawakuwa wengi zaidi, kifupi muamko wa mashabiki kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly ulikuwa kawaida.

Lakini pia Yanga sc waliingia wakiamini wanaenda kupata alama tatu muhimu ili kuandaa mazingira ya kukusanya alama nyingi ili kusonga hatua inayofata, lakini pia hilo halikufanikiwa waliishia kupata alama moja.

Yanga sasa hivi focus yao inatakiwa kuwa kwenye michezo iliyosalia kuona namna gani wanaweza kuachanga karata zao ili wasonge hatua inayofata.

Lakini wanatakiwa kujifunza na kuchukua uzoefu kuwa hii michuano ya klabu bingwa watu hawaangalii unachezaje wanaangalia unakusanya vipi alama, actually you can play good football but good football without a positive results inaboa.

Sitoshangaa Yanga sc wasipotinga hatua inayofata kwasababu hata malengo yao pia msimu huu ilikuwa ni kutinga hatua za makundi tu, ingawa pia nitawapongeza kama mwalimu atafanya turn up kwenye mechi zilizosalia na kuona namna ya kuipeleka Yanga sc hatua ya robo fainali.

NB.Tumaini pekee kwa Yanga sc kutokana na ugumu wa kundi hili ni Yanga sc kuhakikisha anapata alama zote sita za mechi mbili za nyumbani na kucheza vizuri away.

Ameandika mchambuzi nguli wa michezo wa Clouds Media Mkazuzu kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Makala Nyingine

More in CAF Champions League