Connect with us

NBC Premier League

NAMUNGO,DODOMA JIJI HUKO RUANGWA HAPATOSHI LEO

Timu za soka za Namungo na Dodoma Jiji leo zitamenyana vikali kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kusaka alama 3 muhimu kwa timu zote mbili kuelekea kwenye malengo yao ya msimu huu.

Namungo watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Majaliwa kuwaalika walima zabibu hao kutoka Dodoma kwenye mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani wa aina yake huku ukichagizwa zaidi na matokeo ya michezo ya mwisho na hata nafasi zao.

Wakati Namungo wanaoshika nafasi ya 12 wakiwa na alama zao 11 baada ya michezo 11 wametoka kupoteza 1-0 dhidi ya Geita Gold Gold lakini wageni wao wakitoka kupoteza kwa matokeo kama hayo [1-0] dhidi ya Wajelajela Tanzania Prisons wakiendelea kusalia nafasi ya 7 wakiwa na alama zao 15.

Pamoja na yote hayo muamuzi sahihi ni Muda. Mchezo huu unatarajiwa kuwa mubashara majira ya saa 11 jioni.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League