Connect with us

CAF Champions League

WALIOVUNJA VITI UWANJA WA MKAPA KUKAMATWA.

Jumamosi ya wiki iliyopita klabu ya Young Africans ilicheza mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Al Ahly katika dimba la Benjamin William Mkapa.

Baada ya mchezo huo kuna video ilikuwa inasambaa mitandaoni ikiwaonyesha mashabiki waliojitokeza kutazama mchezo huo wakifanya vurugu kwa kung’oa viti jambo ambalo limemuibua Naibu Waziri wa sanaa, Utamaduni na Michezo Mh. Hamis Mwijuma.

Naibu Waziri mwenye dhamana ya michezo Hamis Mwinjuma [Mwana FA] amesema vitendo vilivyofanywa na baadhi ya mashabiki cha uvunjaji wa viti kwenye dimba la Mkapa baada ya mchezo wa Yanga dhidi ya Al Ahly ni cha kihuni na ameiona video inayosambaa mitandaoni hivyo kwa sasa uchunguzi unafanyika na watakaobainika hatua zitachukuliwa dhidi yao.

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1 mwishoni mwa wiki iliyopita goli la Al Ahly lilifungwa na Percy Tau huku goli la kusawazisha kwa upande wa Yanga likifungwa na Pacome Zouzoua.

Klabu ya Yanga kwasasa inajiandaa na safari kuelekea nchini Ghana kwaajili ya mchezo wa tatu wa Ligi ya mabingwa Barani Afrika dhidi ya Medeama.

Yanga ina alama moja pekee na ipo mkiani mwa msimamo wa kindi D linaloongozwa na Al Ahly yenye alama nne [4] zikiwa timu zote zimecheza michezo miwili [2].

Makala Nyingine

More in CAF Champions League