Connect with us

NBC Premier League

FEISAL MCHEZAJI BORA NOVEMBER.

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Azam, Feisal Salum ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi November 2023 akiwashinda Kipre Junior wa Azam na Maxi Nzengeli wa Young Africans.

Feisal katika mwezi November alifunga magoli mawili [2] na kutoa pasi za usaidizi wa mabao nne [4].

Upande wa tuzo ya kocha bora wa mwezi ni kocha mkuu wa Azam fc Bruno Ferry aliyeiongoza Azam fc katika michezo mitatu [3] na ikaibuka na ushindi michezo yote akimshinda Miguel Gamond wa Yanga na Heron Ricardo wa Singida FG.

Kamati pia imemchagua Nassor Makau, meneja wa uwanja wa CCM Mkwakwani, Jijini Tanga kuwa meneja bora wa uwanja kwa mwezi November.

Makala Nyingine

More in NBC Premier League