Connect with us

Timu za Taifa za Wanawake za Tanzania

TWIGA STARS YAFUZU WAFCON 2023.

Timu ya Taifa ya wanawake ya Tanzania imefuzu kushiriki fainali za mataifa ya Afrika kwa upande wa Wanawake baada ya kuiondosha timu ya Taifa ya Togo kwa jumla ya magoli 3-2.

Twiga Stars iliibuka na ushindi wa 3-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika Dimba la Azam Complex, Chamazi, na katika mchezo wa pili wakapoteza kwa jumla ya magoli 2-0.

Twiga Stars sasa itaipeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya WAFCON mwakani nchini Morocco.

Hii ni mara ya kwanza kwa timu mbili za Taifa kutoka Tanzania kushiriki katika fainali za mataifa ya Afrika kwa pamoja baada ya Taifa Stars kufuzu kushiriki fainali za AFCON 2023 zinazofanyika nchini Ivory Coast.

Makala Nyingine

More in Timu za Taifa za Wanawake za Tanzania