Mchambuzi wa soka nchini Tanzania Tanzania Farhan Kihamu amesema mahali ambapo Young Africans imefika msimu huu hakuna kitu wanachodaiwa kwani wametimiza malengo waliyojiwekea mwanzoni mwa msimu huu wa Ligi ya mabingwa Afrika.
“Kama una ndoto ya kuingia makundi Klabu bingwa Afrika , ni mara chache sana unaweza ukaenda nje ya makundi ! Kama una ndoto ya kufika fainali maana yake utajiandaa kuwekeza kwa fainali ,mafanikio makubwa zaidi utakayoyapata itakuwa ni Nusu fainali au Robo fainali “
“Ukisema una ndoto ya kubeba taji ,maandalizi yako yanaweza yakakupa Nusu Fainali au Fainali “
“Yanga wao wanasema target yao ni makundi , unakubaliana nao kwa sababu ni timu ambayo inajitafuta kwenye mashindano ya Afrika , malengo yao waliyojiwekea hawana wanachodaiwa “
“Sioni kwenye lile kundi kama Al Ahly malengo yake ni kuishia makundi ,CR Belouizdad simuoni makundi , Medeama pia huwezi kuliona hilo , wakati mwingine unalaumu malengo waliyojiwekea “
“Unapozungumzia Champions league maana yake ni ligi ya mabingwa , mabingwa wanapokutana wanashindana”
“Kwa malengo ya Yanga, siwaoni wakienda hatua ya ziada kwenye makundi ,mimi binafsi naona Yanga hapa kwenye makundi kwa hali ilivyo ,msimamo na timu zilizopo nawaoma Yanga waki-struggle kwa sababu ya malengo waliyojiwekea “
“Wanaposema hatua ya mtoano ni bonus,inaenda kwa mashabiki na wachezaji hawataokuwa na upambanaji wa ziada kutoka pale kwenda mbele”
Klabu ya Young Africans imesafiri kuelekea nchini Ghana kwaajili ya mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Medeama utakaopigwa Ijumaa wiki hii.
Yanga ipo mkiani mwa msimamo wa kundi D ikiwa na alama moja pekee katika michezo miwili waliyocheza, ikitoa sare moja na Al Ahly huku wakipoteza ugenini dhidi ya CR Belouizdad.