Connect with us

NBC Premier League

TATHMINI YA MCHEZO : SINGIDA FG V KMC

Sare ya 2-2 dhidi ya JKT Tanzania ndio matokeo kumbukizi wanayoingia nayo Singida FG kwenye mchezo wa leo dhidi ya KMC. Mchezo uliopigwa kwenye dimba ambalo limefungiwa hivi sasa la CCM Liti huku goli lao la kuswazisha la pili likizua sintofahamu.

Singida FG wamekuwa na nyakati nzuri hivi karibuni kwani kabla ya sare na JKT walitoka kushinda 2-1 dhidi ya Coastal Union.

Wakitumia zaidi mfumo wa 4-3-3, Habibu Kiyombo amekuwa kwenye kiwango bora hadi kutwaa mchezaji bora wa mwezi lakini ni namna pia pamekuwa na mpishano mzuri wa safu ya ushambuliaji akiwemo Duke Abuya, Marouf Tchakei/Meddie Kagere na Kyombo lakini Morice Chukwu, Kagoma na Bruno kwenye Kiungo wamekuwa Bora pia.

KMC wametoka kuchakazwa 5-0 na Azam kwenye mchezo wao wa mwisho huku pia wakishinda 3-2 dhidi ya Mashujaa kabla ya kipigo hiko.

Moalin amekuwa muumini sana wa vijana lakini kwenye michezo ambayo inahitaji ukomavu zaidi vijana wake hawajawa na msaada sana hasa kwenye mechi kubwa na ndicho kilichotokea hasa kwenye mchezo dhidi ya Azam. Ni vita za mmoja kwa mmoja walkzoshinda Azam ndizo zilizowapelekea dhahma hiyo.

Bahati mbaya wanakutana na timu nyingine yenye wachezaji wakubwa na wazoefu pia hasa kwenye matumizi wa nafasi. KMC wanapaswa kuwa makini sana hasa maeneo ya pembeni. Mchezo uliopita upande wa Boniface Maganga ulitumika sana kama njia ni sehemu ya kwanza Mwalimu Moalin kuangalia anaparekebisha vipi.

Vita ya alama 3 leo ni kubwa sana kwa timu hizi zinazoshika nafasi 4(Singida FG) na ya 5(KMC) zikiwa na alama 19 zote kwenye kupigania nafasi 4 za juu. Lakini kutopata matokeo mazuri kwenye michezo iliyopita itanogesha zaidi mchezo wa leo.

WA KUANGALIWA

SINGIDA FG : HABIBU KIYOMBO; Amekuwa kwenye kiwango kizuri hivi karibuni akifunga mabao lakini pia kutengeneza nafasi.

KMC : WAZIRI JUNIOR ; Anaweza kuwa kimya kwa dakika nyingi za mchezo lakini ni mshanbuliaji hatari na anaweza kujitengenezea nafasi pia.

UWANJA : BLACK RHINO ACADEMY, KARATU

MUDA : SAA 10 JIONI

Makala Nyingine

More in NBC Premier League